Monday, December 10, 2012

CHECK OUT: SWAHILI FASHION WEEK NDANI YA GOLDEN TULIP




 


CHECK OUT: AFTER SCHOOL BASH ILIVYOTISHA NDANI YA MBALAMWEZI BEACH

                                                                      Mashabiki
                                                                      Mwana FA
                            Baba John akiwa na mtu ambaye amefanana na Diamond Platinum
          Huyu ndiye ameibuka kuwa mshindi wa kufanana na mimi dzain tumetokelezea
                                                                   Kala Jeremiah
                                                                       B Dozen
            Kala Jeremiah akiwa na shabiki wake ambaye atafanya naye remix ya Dear God
                                                                      Godzilla
                                                                            Weusi

                                                                            Shetta
                                                                       Country Boy
                                                               Team D'Wikend Chart Show
                                                                    DeeAndy na Cloud
                                                            Tash akionyesha vitu vyake
                                                                   Tumetokelezea
                                                  Warembo ndani ya After School Bash
                                                                   Team Kankaraga
                                                                     Linex Sunday
                                                                    Team G5 Click
                                                               Dj PQ na Dj Choka
                                                                       Mwana FA
                   Walter Chilambo mshindi wa Epiqbss akionyesha vitu vyake kwenye stage.
                                                     Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee

                                                                DeeAndy na Millard Ayo
                                                                   Tumetokelezea
                                                                        Stamina
                                                                      Bob Junior
                                                                 Dj Zero on 1 n 2
                                                                          Mr Blue
                                                       Adam Mchomvu kwenye stage
                                                                         Joh Makini
                                                                         Team Caston

Friday, November 30, 2012

WATU WANNE WALIYOMUIBIA NGUO NA KUMKATA VIDOLE SHARO MILIONEA WAKAMATWA....

Watu wa nne wamekamatwa na jeshi la police wakiwa na Baadhi ya vitu alivyokuwa navyo marehemu Sharo Milionea kama vile Jeans,T-Shert,Viatu,Simu ya mkononi,Pete,Cheni,Tairi moja la gari,pamoja na Battery la gari alilopatanalo ajali marehemu Sharo Milionea....Inasemekana watu hao waliposhindwa kumvua Pete vidoleni walimkata vidole vyake....Watuhumiwa hao walikuwa sita wamekamatwa wanne bado wawili waliokimbia na pesa alizokuwa nazo Maremu Sharo Milionea....

Wednesday, November 28, 2012

  1. CHUKUA TAHADHARI KABLA HATARI

Habari ya kweli iliyotokea wiki iliyopita.
Kuna dada mmoja anasoma chuo buguruni na pia ni mfanyakazi hivyo jioni akitoka kazini ndipo huenda shule.Sasa akiwa njiani kuelekea chuo akapigiwa simu na mtu asiyemfahamu akajitambulisha kwamba yeye ni daktari wa lugaro hosp na kumuulizia habari za mwanae ambae alishawahi kwenda kumtibu pale na chakushangaza zaidi akataja mpaka aina na rangi ya nguo aliyovaa siku ile alipokwenda hapo hospitali na yote yalikuwa kweli.
 Na zaidi akamwambia najua sasa hivi unaelekea chuo buguruni na kweli ilikuwa hivyo, lakini mwishoni akamweleza kwamba kuna mambo anataka kujua kujua kuhusu hicho chuo hivyo nae anaelekea huko hivyo akifika tu atamtafuta. Kwa muda wote huo huyo dada hakuweza kabisa kumkumbuka ila akajipa moyo kwamba yamkini huyo mtu atakuwa  anamfahamu vizuri.
Baada ya kutoka chuo akiwa na wenzake watatu akawa anawasimulia habari za huyo mtu ndipo simu yake ikaita,kupokea yule mtu akamwambia nakuona uko na wenzio wawili mnavuka barabara na kumueleza jinsi alivyovaa sasa wenzie wakasema huyo mtu anakufahamu haiwezekani hapa tupo watatu kweli na ameweza kukutambua. Kisha huyo mtu akamwelekeza mahali alipo ambapo haikuwa mbali na barabara.
Lakini alipomtazama hakumfahamu kabisa, basi akampa mkono kumsalimia, baada ya hapo hakujitambua na zaidi alijikuta yuko maeneo ya chuo kikuu cha DSM akiwa hoi. Kuangalia simu na kila kitu chake kilikuwa salama na hakufanyiwa kitu chochote, kwa bahati kulikuwa kuna ndugu yake anasoma chuo hivyo akawasiliana nae ili kupata msaada ikabidi awahishwe mwananyamala hosp lakini ikaonekana sumu iliyotumika ni kali na dawa yake wanayo regency hosp,hivyo akawahishwa regency na kupata matibabu.
Baada ya ufahamu kumrudia akakuta mtu huyo kachukua pesa zote kwenye mpesa,tigo pesa na bank ( NMB na CRDB) kiasi cha milioni 3, hivyo inawezekana walipompa sumu alitaja password pasipo kujijua.
Na bank walipotazama kwenye ATM Camera waliona picha ya huyo mtu na yeye alimkumbuka vizuri, lakini polisi Kijitonyama wakakiri kwamba kesi hizo sasa hivi zimetokea mara nyingi na huo mtandao ni mkubwa, walipoenda kwenye usajili wa simu walikuta ni huyo huyo na jina lake ndilo alilojitambulisha.Ingawa polisi wameshindwa kumkamata.
Akiwa kituo cha polisi mara huyo mtu akampigia simu akimwambia ‘’kumbe wewe ni muoga sana tutakurudishia pesa zako’’. Sasa kumbe wanachofanya wanakuambia’’ tutafutie mtu ambae unahisi ana pesa kuliko hizi  halafu tukifanikiwa tutarudisha pesa zako’’ hivyo inawezekana nae kuna mtu anaemjua alifanyiwa hivyo akaamua kumtaja yeye