Monday, November 12, 2012

DIAMOND AGUNDUA KITU BAADA YA WALTER KUWA MSHINDI WA EPIQ BSS

Msanii wa kizazi kipya hapa Tzee almaarufu kama Diamond Platinum wa wasafi baada ya kutamba na ngoma zake kali na kupelekea kuwa na mashabiki wengi hapa Africa sasa
Latest Info kutoka kwa msanii huyu ni kwamba leo kupitia katika mtandano wake ameweza kuandika kwamba amegundua kitu kwa msanii wa Epiq Bss baada ya kutwaa ushindi na huu ndiyo ujumbe kutoka katika mtandano wake unaojulikana kwa jina la This is Diamond huyu hapa anafunguka kama hivi"Kiukweli muda wangu uwa ni mchache sana kukaa kwenye TV,ila siku ambayo Walter aliimba wimbo wa Mawazo nilikuwa home.....nikamsikiliza kwa umakini sana nakugundua anakitu ndani yake, namaanisha ana uwezo wa ziada na nafasi nzuri katika muziki wa Tanzania, swala la kufika level za kimataifa hilo ni swala la sisi watanzania kumwezesha pamoja na Yeye kuwa under management makini hasa kipindi hichi anachoanza kuingia katika fani hii ya muziki....nilimpigia kula nikijiamini Walter ndiye mshindi wangu na kweli hajaniangusha....Nimefurahi sana. Nakutakia kila La Heri.Huo ndiyo ujumbe kutoka kwa Diamond baada ya kumkubali Walter.

No comments:

Post a Comment