MFANYABIASHARA SUBASH PATEL ACHANGIA BATI 300 ZA THAMANI YA ZAIDI YA TSH M 8 UJENZI WA MABWENI KILOLO IRINGA
| Bati 300 zenye thamani ya Tsh. milioni 8 zilizotolewa na Subash Patel wilaya ya Kilolo mkoani Iringa |
BAADA
ya mfanyabiashara na kada wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa
Iringa Salim Abri Asas kukabidhi mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya
zaidi ya
shilingi
milioni 3
,mfanyabiashara maarufu nchini Subash Patel ameungana na Asas kwa
kuunga mkono jitihada za mkuu wa wilaya ya kilolo katika mkoa wa
Iringa Gerald Guninita kwa kwa kuchangia bati 300 zenye thamani ya
zaidi ya shilingi
milioni 8 ili kusaidia kukamilisha ujenzi huo wa mabweni zaidi ya 8
yanayoendelea katika wilaya hiyo
Patel
ambaye ni mkurugenzi mtendaji wa kampuni ya M.M.mechangia bati hizo
kama njia ya kuunga mkono jitihada za kunusuru elimu kwa mtoto wa
kike wilaya ya Kilolo na uboreshaji wa elimu wilaya hiyo mpya
ulioanzishwa na mkuu wa wilaya ya Kilolo Bw Guninita.
Mfanyabiashara
huyo ameeleza kuguswa na jitihada hizo zinazofanywa na serikali ya
wilaya ya Kilolo kupitia mkuu wa wilaya hiyo katika kumsaidia mtoto
wa kike kupata elimu bila kurubuniwa na watu wasiopenda maendeleo ya
watoto hao kwa kuwakatisha masomo kwa kuwapa ujauzito.
Hivyo alisema kuwa ili kusaidia ujenzi huo kampuni yake imelazimika kuchangia bati hizo 300 ili
kusaidia kuezeka baadhi ya mabweni ambayo ujenzi wake utakuwa umekamilika .
Akikabidhi
msaada huo leo kwa mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya
ya Kilolo Momahed Gwalima kwa niaba ya mfanyabiashara Patel mkuu
wa wilaya ya Kilolo Bw. Guninita alisema kuwa bati hizo 300
zimetolewa na mfanyabiashara huyo baada ya ofisi yake kutuma barua
ya maombi kwa mfanyabiashara huyo na wengine .
Guninita
alisema kuwa kati ya majukumu aliyonayo katika wilaya hiyo ya
Kilolo ni kuhakikisha anasaidiana na wananchi wa wilaya ya Kilolo
pamoja na wadau mbali mbali wa maendeleo katika kusukuma mbele
gurudumu la maendeleo ya wilaya hiyo ambayo katika mkoa wa Iringa ni
wilaya pekee ambayo bado ipo nyuma kwa elimu.
Kwani
alisema kuwa mbali ya wilaya hiyo ya Kilolo kuwa ni wilaya ina
fursa mbali mbali za kimaendeleo ila bado katika sekta ya elimu hasa
katika suala la mabweni ya wanafunzi ,kilolo ipo nyuma na kuwa
kupitia mkakati huo ulioanzishwa wa ujenzi wa mabweni na vyumba vya
madarasa wilaya hiyo itapiga hatua zaidi katika sekta hiyo ya
elimu.
Mkuu
huyo wa wilaya alisema kuwa mbali ya wilaya hiyo kuwa na shule
zaidi ya
10
za sekondari ila bado wilaya hiyo inachangamoto kubwa ya Hosteli za
watoto wa kike na hivyo kuanza ujenzi wa Hosteli katika shule ya
sekondari mbali mbali wilayani humo.
Bw
Guninita alisema kuwa kwa sasa shule ambazo zitanufaika na
msaada huo ni pamoja na sekondari ya Uhambingeto,Gangwa ,Ukwega na
Masisiwe na kuwa jitihada zaidi zinaendelea kufanyika ili
kuwafikia wadau mbali mbali wa maendeleo katika wilaya hiyo ili
kuweza kufanikisha
harambee hiyo ya ujenzi wa mabweni na Hosteli katika wilaya ya
Kilolo.
Pamoja
na kumshukuru mfanyabiashara Patel kwa msaada wake huo wa bati 300
bado alimshukuru mfanyabiashara Asas wa mkoani Iringa kwa kuchangia
mifuko ya saruji 200 pamoja na mfanyabiashara Yusuf Manji ambae ni
mkurugenzi wa Quality Group kwa kuchangia fedha kiasi cha shilingi
500,000 kwa njia ya hundi kwa ajili ya maendeleo ya elimu wilaya
hiyo ya Kilolo na kuwaomba wadau wengine kuendelea kuchangia zaidi.
Kwa
upande wake mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Kilolo Bw
Ngwalima alimpongeza mkuu huyo wa wilaya kwa jitihada za muda mufupi
ambazo amezionyesha katika wilaya hiyo ya Kilolo na kuwa mkuu huyo
wa wilaya mbali ya kuwa bado hajapata kumaliza hata mwaka mmoja tangu
alipoteuliwa na Rais Jakaya Kikwete ila mambo ambayo amekuwa
akiyafanya katika wilaya ya Kilolo ni makubwa na anapaswa kupongezwa
kwa utendaji wake kazi.
No comments:
Post a Comment