Tuesday, November 6, 2012

MWENYEKITI WA YANGA YUSUF MANJI ACHANGIA ELIMU KILOLO ,IRINGA


MWENYEKITI  wa klabu ya Yanga  Yusuf Manjia(pichani)  amechangia  kiasi cha shilingi 500,000 kwa  ajili ya  ujenzi  wa mabweni ya  wanafunzi  wa  kike katika  wilaya ya  Kilolo mkoani Iringa.

Yusuf Manji ambae ni mkurugenzi wa Quality Group alitoa mchango  huo baada ya  kuombwa na mkuu  wa wilaya ya  Kilolo Gerald Guninita ambaye  pia ni mdau wa michezo hapa  nchini.

Akizungumza na mwandishi  wa habari hizi jana mkuu wa wilaya ya  Kilolo Guninita  alisema kwa pamoja na kumfuta ghafla Manji ofisini kwake  ila hakusita  kujitolea  kuchangia fedha  hizo kwa ajili ya  kuunga mkono elimu ya wilaya ya  Kilolo na kuwa  bila  kuwa na uboreshaji  wa  elimu hata  wanamichezo bora  hawataweza  kupatikana  hivyo  alimpongeza Manji kwa kuwa  kiongozi  wa michezo  wa mfano asiyetazama timu yake  pekee na kuangalia chimbuko la  wanamichezo waliopo mashuleni.

Guninita  alisema  mbali ya Manji wengine  waliojitokeza  kuchangia ni pamoja na  mfanyabiashara na kada wa chama  cha mapinduzi (CCM)  mkoa  wa Iringa  Salim Abri Asas aliyekabidhi  mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya
zaidi ya shilingi  milioni 3 ,mfanyabiashara maarufu nchini  Subash Patel  ameungana na  Asas kwa  kuunga mkono jitihada za   mkuu  wa wilaya ya  kilolo katika mkoa  wa Iringa Gerald Guninita  kwa  kwa  kuchangia bati 300 zenye thamani ya zaidi ya  shilingi milioni 8 ili  kusaidia kukamilisha  ujenzi huo wa mabweni zaidi ya 8 yanayoendelea katika  wilaya hiyo
Petel ambaye ni mkurugenzi mtendaji  wa kampuni ya  M.M.mechangia  bati hizo kama njia ya  kuunga mkono  jitihada za  kunusuru  elimu kwa mtoto  wa  kike  wilaya ya  Kilolo na uboreshaji  wa elimu wilaya  hiyo mpya  ulioanzishwa na mkuu  wa wilaya ya Kilolo Bw Guninita.
Akielezea jitihada  zinazofanywa na wilaya ya  Kilolo katika  michezo mkuu  huyo  wa  wilaya  alisema  kuwa  suala la michezo katika  wilaya ya  Kilolo  limepewa nafasi kubwa na  kuwa  kila  shule  imekuwa ikishiriki michezo na  kuwataka  walimu  kuendelea  kuboresha michezo  zaidi kwa  wanafunzi ila kuwafanya  wanafunzi hao  kuwa na afya bora na kufunguka  zaidi katika masomo yao

No comments:

Post a Comment