Nguzo 22 zaanguka kwa upepo mkali kipawa jijini Dar leo
Shirika
la Umeme Tanzania Tanesco limepatwa na tatizo la kuanguka kwa nguzo 22
za umeme eneo la Kipawa – uwanja wa ndege jijini DSM kulikosababishwa
na upepo mkali uliovuma kutoka eneo linalojengwa uwanja wa ndege wa Mwl,
J.K. Nyerere.
Tatizo
hilo la dharura litasababisha baadhi ya maeneo yote ya kipawa – Tandika
na maeneo ya Temeke kukosa umeme wakati mafundi wa TANESCO wakifanya
kazi usiku kucha.
Njia hiyo ya msongo wa kilovolti 33 unatarajiwa kurudishwa kwenye hali ya kawaida mapema iwezekanavyo.
Shirika
linawaomba wateja wake wote kuwa watulivu wakati mafundi wanahangaika
na linatoa tahadhari kwa mtu yeyote kutogusa waya uliodondoka chini.
Uongozi wa Shirika uanaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kwa raia na wateja wake kwa ujumla.
No comments:
Post a Comment