Thursday, January 10, 2013

OMBA OMBA ALIYEIGIZA MLEMAVU WA MIGUU NA MIKONO ATIMUA MBIO

 Huyu  ni omba omba anayeigiza  kutokuwa na mkono mmoja na mguu akiwa ameka eneo la M.R akisubiri  kuomba chochote  kutoka kwa  wapita njia leo

 Hapa akisubiri msaada  kutoka kwa wasamaria  wema leo
 Hapa akitimua mbio  kukwepa kamera ya mtandao huu leo
Hizi ni kandambili za mzee  janja  huyo

Ule  usemi wa  wahenga  kuwa  ukistaajabu ya mussa utayaona ya filauni leo umetimia katika  eneo la M.R mjini Iringa baada ya  wananchi  waliokuwepo eneo hilo kupigwa na butwaa baada ya mzee janja ambaye amekuwa akishindwa eneo hilo na kujifanya mlemavu asiyekuwa na mkono mmoja na mguu  mmoja kutimua mboni kukwepa kamera ya mtandao  huu.

Tukio  hilo limetokea majira ya saa 8 mchana baada ya camera ya mtandao huo  kufika  eneo  hilo la kushuhudia umati  wa wananchi  wakiendelea  kumpa  fedha mzee janja  huyo ambae alijifanya mlemavu  wa viongo na kuongea kwa  shida .

Hata  hivyo baada ya mmoja kati ya  wananchi kufika  eneo hilo alionyesha  kufichua mbinu hiyo chafu ya  mzee  huyo kujifanya ni mlemavu  wakati asubuhi alikutana maeneo akiwa mzima wa afya  njema na katika  kumhoji zaidi  ndipo kamera ya mtandao huu  ilipoamua  kufanya kazi yake  ya kunasa  kituko  hicho na ndipo mzee   huyo alipoanza  kuongea  kwa  sauti vizuri  tofauti na alivyokuwa akijifanya kuwa hawezi kuongea kabisa (bubu)

Wakati mabishano yakiendelea  eneo hilo ghafla  mzee  huyo alisimama kwa miguu  yake  yote  miwili pamoja na awali kujifanya ni mlemavu asiye na mguu mmoja ila baada ya  watu  kutaka  apigwe  picha ndipo mzee  huyo alipoanza  kutimua mbio  huku ulemavu aliokuwa nao akiusahau hapo  pamoja na kandambili zake na hakuna mtu  aliyeweza  kumfukuza na kufanikiwa  kumkuta.

Baadhi ya  wananchi  wameuomba uongozi  wa Manispaa ya Iringa  kuwabana  omba omba hao ambao  wamekuwa  wakidanganya  watu kuwa  wao ni  walemavu kumbe ni  wazima na kutaka  kuwepo kwa utaratibu maalum wa   watu kuomba misaada.

No comments:

Post a Comment