Sunday, January 27, 2013

PICHA 20 ZA MAANDAMANO YA JANA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ST. JOHN, WALIPOANDAMANA KULALAMIKIA UBAKAJI NA MAUAJI CHUONI HAPO

Huyu jamaa alielala chini ni mtuhumiwa aliekamatwa asubuhi ya leo, ambapo wanafunzi walivamiwa na kuibiwa Laptop kisha wavamizi hao kuchoropoka. Wanafunzi ilibidi wajikusanye muda huo huo na kuwasaka ndipo walipokutana na jamaa huyo ambae alikuwa haeleweki na baadae ikafahamika ni mmoja wao

Basi mtuhumiwa huyo alichukuliwa na polisi kisha wanafunzi waliingia chuoni kuanzisha maandamano

Hapa walikusanyika kwenye bendera kisha kuongea na mkuu wa chuo

Mkuu wa chuo alisema pia nao wamechoshwa na mambo mabaya ambayo wanafunzi wanafanyiwa. Hivyo wanafunzi wawe na subira wanafanya taratibu za kibari cha maandamano ya amani

Wanafunzi baada ya kusubili kwa muda mrefu kibari icho wakaamua kuandaa mabango kwa ajili ya maandamano, ambapo kibari kipatikane kisipatikane walidai kuandamana ni lazima
Basi wanafunzi wakaanza kuchora mabango yao kwa ajili ya maandamano



Mabango yalipokamilika wakasimama kwenye bendera kwa mara nyingine



Walifika mbali na kuona kuwa polisi wanahusika katika mambo mabaya wanayofanyiwa. Ndipo wakachora bango hili kuonyesha hisia zao
Wakaamua kuingia barabarani kwa maandamano baada ya kujaa munkari na jaziba kubwa
Hapa wapo barabarani na masomo kwa siku ya leo hayakuwepo

Bango lina picha ya mwanafunzi alieuliwa kikatili, aliefahamika kwa jina la LYDIA LEO






Ni mchaka mchaka ulioendana na nyimbo za hisia

Magari yalisimama kwa muda mrefu mjini hapo mpaka wanafunzi walipomalizika kupita, kwa hiyo wenye haraka walichelewa

Haya huyu anaashiria demokrasia na maendelea ndio imetawala juu yao

Msafara hapa unaelekea maeneo ya Bungeni

Kila walipopita walikuwa wakishindikizwa na polisi kuhakikisha amani inatawala

Hakuna kitu ambacho kiliniacha hoi baada ya wanafunzi kwenda mpaka Bungeni, kisha walipofika wakaimba nyimbo ya Taifa. Polisi waliwaomba kuongea na viongozi wa maandamano hayo wakajibiwa na wanafunzi kuwa kiongozi wao hameishakufa ambae ni mama LYDIA LEO

Gari la maji ya kuwasha lilikuwepo lakini wanafunzi hao hawakutishika na kitu chochote kile kutoka kwa Polisi



Wanafunzi walifika mpaka Nyerere Square waliimba nyimbo mbalimbali mahala hapo




Baada ya kutembea mji mzima na mabango yao na kuhakikisha kiu yao imekwisha basi waliamua kurudi chuoni

Gari la washa washa nalo lilikuwepo lakini watu walikuwa na jaziba zao vilevile mwanzo mwisho
Barabara zilikuwa zimetawaliwa na wanafunzi kwa kiasi kikubwa, mpaka kusababisha magari kutopita

Hapa ilibidi nipande gari la polisi ili niweze kuchukua picha vizuri, sio siri polisi wenyewe walikuwa wamechoka kwa kutembezwa mji mzima baada kuchat nao kwenye gari ilo

Hapa ndipo safari ya maandamano ilipoanzia na ndipo safari hiyo ilipoishia maeneo haya ya kwenye bendera mbele ya jengo la administration.

No comments:

Post a Comment