TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA ILANI CCM KWA KATA YA KITANZINI MIYOMBONI JIMBO LA IRINGA MJINI
Hapa Jesca Msambatavangu (kushoto) akitekeleza ahadi zake kwa kikundi cha wajasiriamali.
Ndugu wananchi katika uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi vya
siasa ili kushika Dola na kuunda Serikali kila Chama huandaa Ilani yake ya
Uchaguzi.
Ilani hutafsiri na kuelezea Sera zake na kuhusu maeneo muhimu ya
siasa, Uchumi na jamii, na hutoa maelezo fasaha kuhusu mikakati ya utekelezaji
wa sera zinazonadiwa pindi wagombea wake wakifanikiwa kushinda.
Hivyo basi
Chama cha Mapinduzi kilishinda na kushika Dola hivyo ilani yake ndiyo
inayotekelezwa kwa kipindi cha mwaka 2010 hadi 2015.
Mimi pia ni mmoja kati ya wagombea wa CCM kwa ngazi ya kata
yaani Diwani, katika kata ya Miyomboni Kitanzini ambaye nina wajibu wa
kutekeleza ilani hiyo katika ngazi ya Kata hatimaye jimbo kwa kuungana na
madiwani wengine katika manispaa yetu.
Ifuatayo ni taarifa ya utekezaji wa
Ilani ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2010/2012 kwa ngazi ya kata ikiungana na jimbo.
SURA YA KWANZA
MAFANIKIO YA KIUCHUMI
NA KIJAMII MIAKA 5 YA SERIKALI YA AWAMU YA NNE
Katika sura hii inaelezea utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya
Serikali ya awamu ya Nne kipindi cha miaka 5 (2005-2010). Ili lenga katika
kutekeleza kipindi cha pili na cha mwisho cha mwelekeo wa sera za CCM katika
miaka ya 2000-2010. Kwa kuzingatia Dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025 na
malengo ya millennia.
Inaelezea mafanikio yaliyopatikana, kiuchumi, kijamii na
kisiasa.
SURA YA PILI
KUJENGA MSINGI WA
UCHUMI WA KISASA WA TAIFA LINALOJITEGEMEA
Mwelekeo wa sera za CCM katika miaka 2010-2020 umeanisha
jukumu kubwa la Nchi yetu; katika kipindi hiki ni kutekeleza lengo la dira ya
maendeleo ya Taifa 2025 (Tanzania development vision). Ambalo Lengo ni;
“Kuleta Mapinduzi ya Uchumi ulio
nyuma na tegemezi na kuingiza katika mkondo wa uchumi wa kisasa wa Taifa
linalojitegemea”
Ili kutekeleza dira hii ndiyo maana mwelekeo wa CCM kupitia Ilani;
unaiagiza Serikali kutekeleza majukumu kupitia Ilani yake ambayo yatalenga
kutimiza malengo ya millennia na Dira ya maendeleo ya Taifa. Ikiwa ni pamoja na
kujenga Uchumi wa kisasa wa Taifa linalojitegemea yaani modernation ya Uchumi.
Kwa kila ngazi, sasa wote pia kwa pamoja kuanzia ngazi ya mtaa hadi Taifa lazima
tutekeleze malengo haya ya dira ya maendeleo kwa Taifa letu kila mtu kwa nafasi
yake.
KILIMO
Kwahiyo kila sekta kama ni Kilimo wajue lengo ni kujenga
Uchumi wa kisasa utakaopelekea Taifa letu kujitegemea. Wadau ambao ni
wakulima, maafisa ugani au kilimo, wazalishaji wa pembejeo kama mbolea na
mbegu, wauzaji wa pembejeo, vyuo vya mafunzo ya kilimo wote kwa pamoja wajue
tunajenga uchumi wa kisasa utakaopelekea Taifa letu kujitegemea.
Sasa kama
wengine wanazalisha mbegu bora, wauzaji wanachakachuka, wakulima wanapewa mbegu
na mbolea za ruzuku wanauza vocha, Vyuoni hakuna utafiti wakutosha kusaidia
mapinduzi haya ya kilimo ni tatizo katika kufikia mpango wa maendeleo wa Taifa
letu; ambalo tunategemea sisi na watoto wetu waendelee kuishi humu.
Sasa basi Ilani hii 2010-2015 inalengo la Kuongeza KASI ya
ujenzi wa Uchumi wa Kisasa na Taifa linalojitegemea kwa kuwashirikisha na
kuwawezesha kiuchumi wananchi.
Kwa vipi?
Kuongeza maarifa na matumizi ya sayansi na Teknolojia katika
sekta za Uzalishaji. Ili kuongeza Uzalishaji,Ufanisi na Tija au faida katika
uchumi hususani katika:
·
Kilimo
3(31-56) -ndipo ikaanzishwa program ya Kilimo kwanza. Ambayo itaelezea upatikanaji wa Fedha za
uwekezaji katika sekta ya Kilimo; Mbegu bora; Zana za kisasa; Matumizi ya
mbolea; Elimu kwa wakulima kuhusu kanuni za kilimo; huduma za ugani; mikopo kwa
wakulima; upatikanaji wa masoko; utafiti na matokeo; kuongeza thamani ya mazao
ya kilimo.
·
Ufugaji
– Kubadili wakulima kutoka ufugani duni na kuwa wafugaji bora, sio tu wakuhama
hama.
Kutatua matatizo ya malisho na
maji kuwafikisha wafugaji katika ukulima mchanganyiko na ufugaji wa mabandani,
wenye tija kubwa utakao toa nyama na maziwa bora.
Ili kujenga uchumi wa kisasa
na kujitegemea. Ndiyo maana mjini kuna Nyama na maziwa.
Bila mipango hii wale
watoto wetu vichanga wangekunywa nini; hizo nyama choma zingekuwepo.
·
Uvuvi
– Mkazo unalenga katika kuwapatia wavuvi maarifa yatakayobadili na kuongeza
uzalishaji wa samaki.
Samaki wakiongezeka wanaonufaika sio wavuvi peke yao kwa
kupata faida; lakini pia wauzaji wa samaki na walaji wa samaki.
Mwisho uchumi
utaimarika na watu kujitegemea.
Pia Serikali katika hili, inatilia mkazo
uwezeshaji kwa wavuvi, kuendeleza viwanda vya samaki, na kusimamia uvunaji
endelevu wa samaki.
·
Viwanda
– Kutoa msukumo katika mapinduzi ya viwanda; kuhamasisha maendeleo ya Sayansi,
teknolojia, na uhandisi, viwanda vya msingi, kati na vidogo. Ikiwa ni pamoja na
kusimamia viwanda ambavyo tunavyo vya watu binafsi na Serikali.
NB:Mikakati mbali mbali inatekelezwa
kama; MKURABITA, Ushirika, Mfuko wa Pembejeo za Kilimo, Mifuko ya
uwezeshaji,Mfuko wa maendeleo ya Jamii na Benki ya wanawake.
SURA YA TATU
SEKTA YA UZALISHAJI
MALI
KILIMO-3(31-38)
UTANGULIZI
Ndugu wananchi watu wengine wanabeza swala la kilimo kwanza.
Hivi kweli chakula sio kitu cha kwanza katika Nchi? Unaweza ukafanya cho chote
unachofanya kama haujala? Swali huwa
linaulizwa; UNAISHI ILI ULE AU UNAKULA ILI UISHI? JIBU 1.UNAKULA ili UISHI
ndiyo jibu sahihi. 2.Wale wanaobeza Kilimo kwanza ndiyo ambao wangejibu UNAISHI
ili ULE.
Sasa kama watu wote sisi milioni 44 na kitu lazima tule hata
kama ni mlo mmoja kwa siku, nadhani kilimo ni kwanza.Kuvaa unaweza ukavaa nguo
mbili kwa wiki lakini hauwezi kula ugali ule ambao ulisha kula jana ukatoka
tumboni ukala leo.
Hiyo ndiyo maana kilimo lazima kipewe kipaumbele.
Hata kulala utalala kitanda na nyumba hiyo hiyo kwa miaka
mingi lakini sio kula.Na hapo na ufugaji uko ndani yake.
Na kama kilimo hakitiliwi mkazo inakuwaje ninyi hapa sokoni
kila siku wengine tangu wazazi wenu, tangu utoto mpaka mnazeeka mnauza tu
malimbichi zinatoka wapi?
PEMBEJEO ZA
KILIMO-3(32d)
Mbolea za ruzuku na mbegu bora; zimetolewa na hasa ilikuwa
kuwasaidia wale watu wasio na uwezo kabisa, sio kuwatosheleza kuwasaidia. Kata
yetu sisi kutokana na mazingira yake mbolea hizi tumepewa vocha 59 vipaumbele
tuliwapa vijiji zaidi. Na zimetolewa kwenye mitaa yetu yote.
Tatizo pia ni uelewa kwamba wapewe wale wasio na uwezo,
lakini pia wengine wanapewa vocha wanaziuza, shambani hatumii tena, wala shamba
hana.
Lakini pia kuna mbolea za samadi na mboji watu wanaweza kutumia pia.
Uanzishaji wa uzalishaji wa mbegu bora kupitia majeshi lakini
pia, kutoa ruzuku kwenye dawa za mifugo nk.
Sisi kama Kata ya Miyomboni Kitanzini tunanifaika na kilimo
kwanza hasa kwa sababu tuna masoko yote makubwa hapa, ambayo huuza bidhaa za
mashambani, hivyo kutuimarishia uchumi wetu.
UVUVI-3(39)
Kata yetu inanufaika na sera hiyo kwani zaidi ya kupata
kitowe cha Samaki lakini kiuchumi ni biashara yetu. Kwa kweli tunaonga mipango
endelevu kwa uhai wa samaki ili tuendelee kufanya biashara ya samaki.
UTALII-3(45)
Utalii unaendelea kukua katika mji wetu, hata sisi tumeona
faida za moja kwa moja za utalii. Mfano hapa sokoni, soko hili la zamani ni la
kihistoria na lilikuwa soko la kwanza Africa. Ndiyo maana wazungu wanakuja kuja
kula humo ndani kwa akina mama. Akina mama inabidi mjitahidi yes na no
zisiwapige chenga.
Ila nadhani kuna changamoto ya mlango na maji kutiririka
sehemu Fulani na dhani kina mama waseme vizuri ili tuone namna ya kuboresha.
Lakini sisi kata yetu ina hivyo vitu viwili vya kihistoria
kama vivutio vya utalii, ambalo hili soko na Eneo la Kitanzini ambapo walikuwa
wananyongewa watu. Na manispaa imeshaanda mpango wa kupaendeleza ili kutunza
kumbu kumbu hiyo, pamoja na vingine vilivyo ndani ya manispaa.
SURA YA NNE
ARDHI-4(57-59)
Ardhi ni raslimali muhimu katika kuchangia maendeleo. Ina
umuhimu kabla na hata baada yakuendelezwa ili mradi tu ikithaminishwa na
kutambulika kisheria uthamani wake.
Upimaji wa
Viwanja/maeneo 4(60c)
Manispaa kupitia sisi madiwani wake na watendaji, tuliliona
hili kuwa ni hitaji kubwa kwa wakazi wetu kwa ujumla, hasa makazi. Hivyo
tulipendekeza ili kuendana na kasi yakukua kwa uhitaji wa viwanja kunakotokana
na kukua kwa uchumi; ni vyema tukanunua vifaa bora kwaajili ya upimaji. Hivyo
manispaa yetu sasa ina vifaa vya kisasa vya upimaji ambavyo kwa Manispaa zote
Tanzania ni Manispaa mbili tu yenye navyo yaani Arusha na Iringa. Vyenye uwezo
wakupima viwanja 100 kwa siku. Viwanja 400 na zaidi vilipimwa na kugawiwa eneo
la ngelewala, 100 eneo la mafifi, na maeneo mengine yanaendelea kupimwa.
Changamoto tulio nayo ni kutokuwa na ardhi yetu wenyewe.
Ardhi inayopimwa tunaichukua kwa wananchi kwa kulipa fidia, kisha kupima kuwa
uuzia au kuwagawia watu tena. Fidia pia kwa kadri mji ulivyoendelea inakuwa
kubwa kidogo.
Utaratibu wa ugawaji pia umeboreshwa. Kwamba kila fomu
inayotolewa maanake ni kiwanja. Sasa tulichogundua tena wanao kuja kuchukua
fomu zile wengine wanajihimu saa 10.00 usiku, sio wa hitaji wa viwanja wanakuwa
tena madalali.
Kwahiyo kachukua fomu kwa 10,000/= anaiuza 50,000/= mpaka
200,000/=. Sasa hii tena ni shida, cha msingi tunawaomba wananchi muwe mnasoma
matangazo yetu, au kusikiliza matangazo, maana hata kiwanja pia unaweza
ukalanguliwa.
Kuna njia nyingine ambayo mnaweza kupiwa viwanja, kwa kuomba
ofisi za ardhi manispaa ziwapimie kwa kuchingia gharama kwa pamoja. Ila sharti
mtatakiwa mruhusu miundo mbinu yote kupita kwenye maeneo hayo, kama bara bara
nk.
MIPANGO MIJI-4(60b)
Sheria za mipango miji zimeendelea kufuatiliwa, kuzuia ujenzi
holela kati kati ya mji. Natunawaomba wananchi waendelee kufuata sheria za
mipango miji ili kuruhusu kada nyingine kufanya kazi pia bila bughudha.
MKURABITA
Huu ni mpango wa Serikali ya CCM ambao ni mkakati wa
Kurasimisha raslimali na Biashara Tanzania.
Kwa lengo la kutambua rasmi au
kisheria raslimali za wanyonge ambazo bado ziko kwenye sekta isiyo rasmi, ili
zitumike kuwawezesha washiriki kwenye uchumi rasmi wa Taifa. Yaani kutambua
nyumba ambazo zimejengwa katika maeneo yanayoruhusiwa kisheria na taratibu,
lakini hazina hati milki.
Ziweze kukatiwa hati milki ili watu hawa wawe kutumia
nyumba hizo kama corallater au dhamana za kupatia mikopo katika taasisi mbali
mbali za fedha na kuboresha, kuinua au kuanzisha shughuli ya kumuinua mtu
kiuchumi na kisha kujitegemea.
Kwa manispaa yetu ya Iringa chini ya usimamizi
wa madiwani na kwa kushirikiana na watendaji pia, kazi hii itaanzia Kata za
Mwangata, kisha hata Kitanzini tutanufaika na mpango huu wa MKURABITA.
MAJENGO/NYUMBA-4(60a)
Ujenzi na aina ya nyumba zinazojengwa pia ni ishara ya
maendeleo ya kiuchumi ambayo pia huchochea uchumi kuendelea kukua. Nyumba
nyingi zimeboreshwa baada ya manispaa kutunga sheria ya kufungua vichochoro.
Hii imetoa fursa kwa nyumba nyingi kufungua milango ya maduka mengi ambayo
yameinua kipato kwa wenye nyumba na wapangaji pia. Vibali pia vilitolewa kwa
wenye nyumba kukarabati nyumba zao. Na wengine wamepata fursa ya kujenga
maghorofa yameongezeka, hali inayoashiria kukua kwa uchumi.
NISHATI-4(61)
Moja ya matatizo makubwa yaliyikuwa yanavikumba viwanda vyetu
pia, hadi vikapelekea vingi vyake kuzaliza hasara ili kuwa ni upungufu wa
nishati ya umeme. Ikiwa ni pamoja na matatizo ya menejimenti. Hivyo naamini
mwaka huu mgao wa umeme umepungua sana, na kwa mikakati ya mbele pamoja na
upatikanaji wa gesi naamini itatusaidia kutekereza vyema sera ya mapinduzi ya
viwanda.
SURA YA TANO
UWEZESHAJI WANANCHI
KIUCHUMI
Lakini ili wananchi ili waweze kumiliki uchumi lazima wawe na
maarifa ya kisasa. 5(76a) Ilani inasema kufufua kwa nguvu zote elimu yenye
manufaa ya watu wazima nchini kote ili masomo ya ujasiriamali,uwezeshaji,
urasmishaji wa biashara, kilimo, ufugaji na uvuvi yawezekutolewa kwa wananchi
wengi; Hatua za kutoa mafunzo ya ujasirimali lazima zichukuliwe;
Ndugu wananchi ili watu waweze kujenga uchumi wa kujitegemea,
hususani wananchi wa Kata ya miyomboni kitanzini.
Ambayo kwa kiasi kikubwa
imesheheni wafanyabiashara wakubwa na wadogo.
Wanahitaji kupata maarifa hasa ya
Elimu ya ujasiriamali ili kufanya biashara zao kwa ufanisi mkubwa.
Ndugu wananchi, mimi baada yakuliona hilo niliona umuhimu
wakupata mafunzo hayo ya ujasiriamali. Ambayo yalifanyika mara mbili katika
ukumbi wa warfare na Saba Saba CCM. Ambayo yalihusisha 1.utengenezaji wa bidhaa
mbali mbali za viwandani kama utengenezaji wa sabuni za miche, sabuni za maji,
dawa zakuoshea au kudekia, dawa za vyooni nk. 2.Usindikaji wa vyakula mbali mbali.
3.Mafunzo ya ufugaji bora wa mifugo mbali mbali kama kuku na utengenezaji wa
chakula chake, Ng’ombe, mbuzi nk
USHIRIKA-5(76b)
Jumla ya makundi 18 ya watu hamsini hadi sitini
yawajasiriamali yalianzishwa ambao jumla yao ni zaidi ya 1080. Na ofisi yangu
ya Diwani iliwasaidia kuandika katiba na kusajiliwa rasmi manispaa. Vikundi
hivyo ni Mshikamano, Saba saba no.1, 2,3; Nuru Group, Ebenezer Group,
Tuwezeshe, Amani, Nams Group, Juhudi Group nk Pia makundi ya vicoba ambapo
katika Soko la Mashine tatu pekee yake kuna vicoba vitatu. Idadi ya vikundi
vilivyoundwa katika Kata viko zaidi ya 20 na 15 vimesajiriwa tayari na 5
vinaendelea na mchakato wa usajiri. Hivyo jumla ya vikundi vyote 38.
Wajasiriamali pia walielezwa fursa zilizopo zakukopa katika
Taasisi za kifedha zilizopo ndani ya Kata yetu na Nje kama mabenki kama NMB, na
taasisi nyingine kama FINCA, Pride na SACCOS na VICOBA.
Pia walielezwa na kufundishwa namna yakujiwekea pesa au
kusave kama njia mbadala ya kupata mtaji.
AJIRA NA UWEZESHAJI
WANANCHI-5(77)
UBORESHAJI WA MASOKO
Hii pia ni njia mojawapo ya kujenga uchumi, kwani hutoa fursa
kwa wafanyabiashara kuendelea kufanya kazi zao kwa ufanisi mkubwa. Kutokana na
ongezeko kubwa la wafanyabiashara hasa katika kata hii, Manispaa kwa
kushirikiana na wadau wa soko kuu wameboresha soko kuu kwa kushirikiana na
wafanyabiashara. Lakini ili kupunguza msongamano masoko mawili yameongezwa
katika kata hii. Ambalo ni magari mabovu
na mashine
tatu ambalo bado mpango wakuliboresha zaidi, hasa wakati wa masika
unaendelea. Kwani eneo hili linamilikiwa na wenzetu wa Bakwata pia.
Hata hivyo mimi kama Diwani nimeweza kushirikiana na wana
mashine tatu kuhakikisha lile linalowezekana angalau kutunusuru mvua
limefanyika kwa kutoa trubai la kuezekea eneo la matunda.
FURSA ZA KIBIASHARA
VIJANA-5(78)
Ndani ya kata yangu vijana wengi wamenufaika na kuruhusiwa
kwa biashara ya pick-pick alimaarufu boda boda, ambazo zimetoa ajira kwa vijana
asilimia kubwa.
Pia kuna fursa ya Toyo, mikokoteni ambayo kwa kiasi kikubwa
inatupa changamoto ya kuhakikisha bara bara zote zinatumika kwa matumizi
yaliyokusudia ya vyombo vya usafiri.
VIJANA
Mafunzo ya ujasiriamali yalitolewa katika Chuo kikuu RUCO
ambayo mimi mwenyewe niliyatoa kwa vijana wa timu za mbili za mpira wa miguu
kutoka katika kila kata ambazo jumla zilkuwa timu 40 ukiongeza na za vijiji.
Pia mitaji ya mabero ya mitumba nane ili tolewa kwa vijana wa
timu za mpira wa miguu mbili kutoka katika kata ya Miyomboni Kitanzini; ambazo
ni Maghorofani FC na mashine tatu FC.
Pia gunia 10 za mahindi zilitolewa kama mtaji kwa vijana wa mpira wa miguu
Ipogolo United. Na sabuni za kuogea zenye dhamani ya sh.700,000/= zilitolewa
kwa timu ya mpira wa miguu wanawake Ipogolo. Bero kumi za mitumba zilitolewa
kwa vijana wa Iringa Youth club; belo mbili zilitolewa kwa vijana wa kundi la
maigizo kihesa- Umati; Jumla ya fedha taslimu milioni mbili zilitolewa kwa
mabinti walioterekezwa na wazazi au watu waliowapa ujauzito; ambapo
niliwaanzishia kibubu program. Baiskeli zilitolewa kwa watoto wa mitaani na
mafunzo na mashine ya kujzia tyre upepo.nk
Wapiga debe, wasukuma
mikokoteni, makuli, wauzaji wadogo wadogo;
Waliundiwa uongozi na kupewa vitambulisho na unifomu ili
kufanya kazi zao kwa ufanisi. Lakini pia walipewa elimu ya kuepukana na tabia
zinazowafanya wadharaulike katika jamii kama;
·
Wizi
·
Ulevi
uliokithiri
·
Lugha
za matusi
·
Uchafu
Waheshimu kazi yao na kuwa raia wema
na pia washirikiane na polisi kwa ulinzi shirikishi katika maeneo yao. Na
mengine mengi yamefanya kwa vijana hata yaliyo nje na Ilani ya uchaguzi. Kama
kuwasaidia kuwalipia ada za chuo. Kushirikianao katika sherehe zao kama mwaka
mpya nk.
Kushiriki kuzindua kanda au CD zao
katika matamasha mbali mbali. Kuichangia timu ya polisi na mageraza.
Kutelembea wafungwa na kuwa misaada
ya ya sabuni za kuogea 800 na limu za karatasi kumi. Kuchangia mikutano ya
vijana wa CCM, Kuwasaidia hata wale vijana ambao sio wa upande wetu. Kuchangia
uanzishaji wa vikundi wa vya kijasiriamali kama Ipogolo. Kushiriki katika
shughuli za kijamii; kama misiba, harusi, sherehe za vyuo vikuu, makanisa,
misikiti nk.
MIUNDO MBINU
MAWASILIANO na
USAFIRISHAJI/UCHUKUZI
Ndugu wananchi katika kukuza uchumi, mawasiliano ni kitu cha
muhimu, ambayo huwezeza mzunguko wa biashara au huduma kuwa rahisi. 2.(d).
Mawasiliano ya simu za mkononi na hata za meza ndani ya kata yetu hakuna shida.
Watu wanaagiza mizigo kwa simu wanatuma pesa kwa simu. Hivyo imesababisha
kurahisiha ufanyaji wa biashara nakuongeza tija na maendeleo. Hata Kata yetu
haitakuwa na matatizo yo yote kuhama kutoka analogy kwenda digitaly.
BARA BARA
Bara bara zimeimarishwa katika kata yetu na zinapitika kwa
misimu yote kwaasili mia 99% kama sio 100%.
Mapungufu madogo yalipotokea mwaka jana wakati wa mvua kubwa
basi, marekebisho yalifanyika hasa kwa bara bara ya mtaa wa mlimani. Bado
tunachangamoto kwa Bara bara kubwa karibu na eneo la sigara ambalo mara nying
mvua zikinyesha maji hufulika kwa kuwa karavati la eneo lile limetitia hivyo
kushindwa kupitisha maji kwa wingi. Swala hili limefikishwa kwa mamlaka husika
yaani Tanroads na wameahidi kulishughulikia wakati wa mchakato wa kutengeneza
bara bara ya Iringa mpaka Dodoma.
Ununuzi wa Greda
Kwakuona pia mara nyingi bara bara zetu zinaharibika hasa
wakati wa mvua kubwa kama mwaka jana. Nausumbufu unakuwa mkubwa, pia kwakuwa
tulikuwa tunataka kila sehemu tunapopima viwanja angalau tutengeneze njia za
mitaa inayoonyesha jinsi viwanja vilivyogawika.
Basi, tulipendekeza madiwani
ufanyike uchakato wakutafuta greda. Ambao ulianza kwa kurasmisha mali
zetu za manispaa hasa majengo ambayo hayakuwa na hati, ili tupate dhamana
yakutosha kuwekezea ili tuweze kukopesheka. Mchakato ukakamilika hatimaye,
tukakopeshwa fedha na benki ya CRDB ambayo imetuwezesha kununua Greda.
SURA YA SITA
HUDUMA ZA JAMII- ELIMU
MSINGI – 6(85
Ndugu wananchi; ndani ya Kata yetu tuna shule ya sekondari
Miyomboni na sule ya msingi ni Azimio.
Watoto wote wenye umri wa kujiunga na shule ya msingi yaani
miaka saba wamepata nafasi ya kujiunga na shule ya msingi kwa…….asilimia
Ili kubaini matatizo yanayowapata watoto wa shule za msingi
nilifanya nao mkutano. Walitoa kero zao na ziliwasilishwa kwa Mkuu wa Shule;
ikiwa ni pamoja na kuomba walimu wasiuze, vitu darasani. Kwani huwa
vinawapunguzia umakini katika kusoma wanapofundishwa, kwa kufikiri kitu
kinachouzwa na kupopeshwa. Lakini pia huwasababishia kutoroka shule
wakikopeshwa wakakosa hela ya kulipa; huogopa kwenda shule.
Watoto pia waliomba wazazi wao kuwa karibu nao nakupata muda
wa kuwasikiliza wanapokuwa na shida. Hasa kuwapa chai yenye kitafunwa asubuhi.
Akina baba pia wasiwaonee akina mama na akina shangazi.
Kero yao nyingine kubwa ni kutokuthaminiwa hasa kwa
kutowatengea au kuendeleza maeneo ya michezo. Hivyo waliomba mipira na jezi.
Timu mbili za watoto walipewa mipira na jezi, ambazo ni Kitanzini United Stars
na Mshindo wanderous.
WALIMU
Pia walitoa mapendekezo na malalamiko yao huku wakiomba
ushirikiano mkubwa kutoka kwa wazazi; ili kujenga malezi bora.
Wakitoa mfano wakukosa
ushirikiano walisema ni pale walipobaini kuwa mtoto mmoja aliyekuwa akisumbua
sana na mtoro wad rasa la sita alipowajibu amechelewa kwenda shule alikuwa
kuwekwa vipandikizi vya kuzuia mimba. Na hii ilionyesha wazi kuwa mlezi alikuwa
anajua.
Pia walitoa malalamiko
ya baadhi ya changamoto wanazokutana nazo kama wizi uliokithiri kwa maeneo ya
shule, ukarabati wa shule kuwa muhimu, pia nilipata fursa ya kuchangia mahitaji
ya shule hiyo. Pia tuliwaomba polisi kusaidia ulizi wa maeneo hayo. Usimamizi
wa karibu zaidi upo chini ya kata ya mshindo.
SEKONDARI
Kuwa sekondari ya Kata, kuendelea kusimamia ufaulu wa
kuhakikisha zaidi ya asilimia hamsini ya watoto au zaidia wanafaulu na kujiunga
na kidato cha kwanza ifikapo mwaka 2015. Kiwango cha ufaulu kwa watoto wetu
Miyomboni kimekuwa kikiongezeka kwa……….
UJENZI,
Ilani inatakakuendelea kuboresha shule kwa ujenzi wa maabara,
madarasa, vyoo, nyumba za walimu, nakununuavifaa vya shule.

No comments:
Post a Comment