TEJA AKUTWA AMEKUFA KWA KUJIDUNGA MADAWA YA KULEVYA
| Nyumba ambayo mwili huo umekutwa |
| mwili wa kijana Stan Mhepelwa ukiwa katika gari ya polisi leo |
| Bomba la sindano lililokutwa katika chumba hicho |
| Mwili wa kijana huyo ukitolewa Kijana anayesadikika kuwa mtumiaji wa madawa ya kulevya (teja) mjini Iringa Stan Mhepelwa mkazi wa Ilala katika Manispaa ya Iringa amekutwa akiwa amekufa katika nyumba ambayo bado kukamilika eneo la barabara mbili katika Manispaa ya Iringa. Mashuhuda wa tukio hilo wameueleza mtandao huu wa www.francisgodwin.blogspot.com kuwa tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo jumapili ambapo mwili wa kijana huyo umekutwa mida ya saa 3 asubuhi na wananchi waliokuwa wakipita eneo hilo . Samson Kalinga ni mkazi wa eneo hilo amesema kuwa nyumba hiyo imekuwa ikitumiwa na vijana hao mateja kama sehemu ya kujificha na kujidunga madawa ya kulevya kwa kutumia sindano na kuwa chanzo cha kifo cha kijana huyo kinasadikika kuwa alijidunga sindano vibaya . Hata hivyo alisema mwili wa kijana huyo umekutwa katika chumba hicho huku pembeni kukiwa na mabomba ya sindano na kuwa aliyetoa siri ya kifo cha kijana huyo ni teja mwenzake ambae alikuwa akiingia katika chumba hicho ili kuendelea kutumia madawa ya kulevya. |
No comments:
Post a Comment