Friday, January 18, 2013

WALIOIBA MAMILIONI YA SHILINGI MUFINDI WAREJESHA

 Bw. Limbakisye Shimwela akiwa na baadhi ya makombe ya tuzo mbalimbali za ushindi katika ofisi yake.

HATIMAYE  fedha  za serikali zaidi ya sh. Milioni 109 zilizoibwa na baadhi ya wafanyakazi wa banki kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, zimerejeshwa, baada ya uongozi wa uongozi wa Halmashauri.
 Wizi huo wa kitaalamu uliofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa  taasisi ya kifedha hapa nchini (NMB) ya Wilaya ya Mufindi Mkoani Iringa, kwa kushirikiana na baadhi ya watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, na kuchepusha  fedha za Halmashauri hiyo zaidi ya Shilingi Milioni 109 kwa manufaa yao binafsi.
Wakizungumzia sakata hilo katika kikao cha baraza la madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi, kilichokaa kujadili masuala mbalimbali ya maendeleo, pamoja na wizi wa fedha hizo, ambapo Madiwani walisema licha ya watumishi hao kurudisha fedha hizo lakini taratibu za kisheria zinapashwa zichukuliwe dhidi yao ili iwe fundisho kwa wengine.
Akichangia hoja ya fedha hizo za Umma, Evaristo Luhunga diwani wa Kata ya Ikweha alisema watumishi hao wanatakiwa kupewa adhabu licha ya kurejesha fedha hizo, kwani wamechangai kudumaza uchumi wa Halmashauri na wananchi wake.
“Hatua hii tuliyofikia inadhihirisha wazi juu ya kazi kubwa tulioyoifanya katika kufuatilia fedha hizi, lakini nisingependa tuishie hapa, kwani   watumishi wengi wamekuwa wakicheza na fedha za umma, lakini nini madhara ya wizi wa fedha hizi za wananchi, kuna haja ya kuwachukulia hatua za kisheria, ili iwe fundisho kwa watumishi wengine wenye tabia kama hizi,” Alisema Luhunga.
Naye Ernei Nyeho diwani wa Kata ya Mdabulo amesema inapotokea fedha zilizopitishwa na baraza la madiwani kwa ajili ya kukamilisha miradi mbalimbali halafu watu wachahe kwa maslahi yao binafsi wanachukua, watu hao wanatakiwa kuchukuliwa hatua kali za kisheria.
“Mimi katika Kata yangu fedha hizi zililenga kuboresha mradi wa elimu na afya kwa kununua madawati pamoja na kujenga madarasa, lakini siyo tu kwenye kata yangu, tatizo hili limeyumbisha uchumi wa Halmashauri nzima,” Alisema Nyeho.
Akitaja majina ya watumishi waliochepusha fedha za umma , mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Limbakisye Shimwela  amesema  waliohusika ni Alan Leonard, Paulo Mwaluko pamoja na Willium Fwimi wote wakiwa ni watumishi idara ya uhasibu.
Aidha Shimwela  amewataka watumishi wote kuwa na nidhamu katika    kazi na uaminifu katika fedha, ili kufanikisha mpango wa kuleta maendeleo ya wananchi na taifa kwa ujumla.

“Hakuna kitu kizuri katika kazi kama kuwa muumini wa uadilifu, unajua unapopewa dhamana si kama wale wengine wasio na cheo kama chako hawana akili au hawana uwezo huo, bali Mungu amependa tu wewe kuwa hivyo, kwa hiyo unatakiwa kufanya kazi kwa uaminifu mkubwa ili kujenga imani kwa wananchi unaowatumikia,” Alisema Shimwela.

Amesema fedha za idara ya elimu msingi shilingi Milioni 45 zitachonga madawati  600  ambayo yatagharimu shilingi Milioni 27, kwa  shule 20, huku kila shule ikipatiwa madawati 30.
Na   shule  Milioni 18  zitakarabatiwa miundombinu ya barabara  kwa shule 6 ambazo zimekuwa kikwazo kikubwa kwa wanafunzi na walimu kufika shuleni, na kujenga nyumba ya mwalimu iliyokuwa imenguka katika shule ya msingi Nandala.
Ambapo shule za sekondari zitaboreshewa maabara 8 (Mobil Laboratories) zitakazogharimu jumla ya shilingi Milioni 48 ili kuwawezesa wanafunzi wa masomo ya Sayansi kufanya vizuri kwa kupatiwa mafunzo kwa vitendo.
Na milioni 7 ikikamilisha Bweni la wanafunzi wa sekondari ya Ilogombe na Milioni 8 zikipelekwa katika idara ya afya na hivyo gharama ya shughuli hizo kukamilisha jumla ya  shilingi Milioni 109 ya fedha zote ambazo zilikuwa zimeibwa.

Hata hivyo wananchi wameupongeza uongozi wa Halmashauri hiyo,   ukiongozwa na kusimamiwa na Mkurugenzi wake Bw. Limbakisye Shimwela kwa kufanikisha fedha hizo kurejeshwa na hivyo kuchangia shughuli za maendeleo na uchumi.

No comments:

Post a Comment