Friday, February 1, 2013

OMBA OMBA IRINGA WAJA NA MBINU MPYA YA 'KIDIGITALI' KATIKA KUOMBA ,SASA WASHINDA KTK ATM

 Hapa mwanamke  huyo ambae ni omba omba maarufu mjini Iringa akimsubiri mteja wa benk ya NMB aliyeingia  kutoa  pesa katika ATM eneo la  ofisi ya Manispaa ya Iringa  ili aombe  pesa
Hapa mteja huyo akitoka   huku omba omba  huyo akimwomba pesa .

WATU  wanaofanya kazi ya  omba omba  katika manispaa ya Iringa mkoani Iringa  wamejigungulia mbinu mpya  ya  kuomba  pesa kwa  watu mbali mbali baada ya kuona kasi ya  wananchi kuwasaidia  kupungua na idadi ya omba omba ikiongezeka  na  hivyo ili  kupambana na wale wenye tabia ya  kusema sina pesa ,sasa omba omba  wameamua  kukaa maeneo yenye mashine  za kutoa fedha (AMT ) ili  kufanya shughuli hiyo.

Mmoja  kati ya omba omba maarufu mjini Iringa ambae  hakupenda  kutaja jina lake alisema  kuwa   wameamua  kubuni  mbinu  hiyo  baada ya  wananchi  nao  kubuni mbinu ya  kuwanyima  pesa  kwa kila anayeomba  fedha hata kama mfukoni ana pesa bado amekuwa akiwanyima kuwa hana pesa.

" Tumeamua  kuboresha huduma  yetu   zaidi  kuhama katika mfumo  wa  zamani ya analojia na kujiunga na mfumo mpya  wa Digitali kwa  kusogea katika mashine za ATM kama unavyoona  sasa wengi wetu  tunawasubiri  wasamaria  wema katika mashine" alisema  mwanamke  huyo


Hata  hivyo  alisema  sababu nyingine ya  kuondoka barabarani ambako  awali  walikuwa wakijipanga kuomba  fedha  ni kutokana na idadi ya omba omba  kuongezeka zaidi katika barabara mbali mbali za mji  wa Iringa hivyo  kukosa fedha ya maana na  wengi  wao kujikuta  wakirejesha majumbani kwao bila kupata  hata senti moja.

Alisema  kuwa  mbinu  hiyo ya kusogea katika mabenki ya katika mashine za ATM umeanza  kuzaa matunda kwao  kutokana na  sehemu kubwa ya  omba omba  kutojua  kusoma hivyo wamekuwa hawajui kama katika mashine  hizo ndiko  watu wanakotoa  fedha  hivyo kwa wale  wajanja  wamekuwa  wakipata  zaidi kwa  kuwafuata watumiaji wa ATM katika maeneo husika .

"ujue mwanangu  hapa katika ATM mtu kukunyima anaona aibu  kwani tayari  umemwona anachukua pesa na  pili hawezi  kukupa chenji  chenji kwani mashine hizi hazitoi chenji  ....ila ukikaa barabarani   wanakupa shilingi 50 ama 100 sasa unaweza  kutwa nzima ukashindia 2000 wakati hapa katika ATM unaweza  kupata hadi shilingi 50,000 kwa siku .....sasa  anglia mwenyewe wapi panafaa" alihoji omba omba  huyo.

Wakati  omba omba  hao wakionyesha ubunifu mkubwa katika  kazi hiyo baadhi ya  wananchi  wa Manispaa ya Iringa  wameutaka uongozi  wa Manispaa ya Iringa na mkoa  kuigilia kati suala la kuongezeka kwa omba omba  hao na  kuwa wapo baadhi ya  watu  wamekuwa  wakidanganya kama ni omba omba  kumbe wa  watu wenye familia  zenye uwezo .

Huku baadhi yao  wakiingiza kuwa ni  walemavu  wa  viungo kumbe  ni matapeli  wanaoigiza ulemavu ili kujipatia  fedha na  wanaponyimwa  fedha  wamekuwa  wakiwatukana wale  wanaowanyima matusi ya nguoni ama hata  kutaka  kuwapiga.

No comments:

Post a Comment