Friday, September 13, 2013

HATUA ZA KUJIONDOA KATIKA MAGROUP USIYOYAPENDA KATIKA FACEBOOK


Katika mtandao wa kijamii wa facebook, kuna makundi (Groups) mengi ambayo mtumiaji wa mtandao huu anajikuta ameunganishwa hata pasipo kujijua. Na hii inakuwa kero maana unakua umeunganishwa kwenye group ambalo huna 'hobby' nalo kabisa. Kwa mfano watu wengine si wapenzi wa siasa, na unakuta umeunganishwa kwenye group la mambo ya kisiasa. Unajikuta unakereka vibaya sana. Lakini katika zama hizi huna sababu ya kukereka. Maisha haya tunapaswa kuishi kwa amani na furaha. Fuata hatua zifuatazo kujitoa kwenye ma-group usiyoyapenda.
Hatua ya kwanza:
Kwenye upande wako wa kushoto wa akaunti yako click kwenye groups. Itakuleta moja kwa moja kwenye window yenye magroup yote ambayo ulishawahi kujiunga au kuunganishwa na mtu. Window hyo inawezekana ikaonekana kama hii:

 Hatua ya pili:
Kwenye window ya hayo ma-group, kolamu ya kwanza kabisa inaka 'feature' ka-'edit'. Click kwenye edit. 
 Ukisha click hapo itaonekana window kama hii hapa chini:
Hatua ya Tatu:
Itakuuliza uthibitishe. Basi click leave the group
 Basi ukifanya hivyo facebook itakuondoa kwenye kundi au group hilo.
Ndivyo unavyopaswa kufanya mara kwa mara ili ukurasa wako wa facebook uwe msafi na hakikisha unatoa notifications ya status na tags zisiwe zinakuja kwenye email yako moja kwa moja.
Hii ndiyo teknolojia yetu.

No comments:

Post a Comment