IJUE MITANDAO YA KIJAMII YENYE WATUMIAJI WENGI ZAIDI DUNIANI
Kuibukia kwa mitandao ya kijamii
kumebadilisha sana matumizi ya mitandao duniani. Kabla ya kuibukia kwa
mitandao ya kijamii mitandao ilikua na taarifa muhimu sana lakini ambazo
kulikua na mwanya mdogo sana wa wasomaji na watumiaji wa mitandao
kuweza kuchangia mawazo yao. Leo mitandao ya kijamii imetimiza matumizi
halisi ya mitandao: kuunganisha binadamu wote duniani. Kwa kuunganishwa
huku mitandao ya kijamii inamsaidia mtumiaji kuweza kujua mtumiaji
mwingine, amejiungaje na amejiunga na akina nani. Kwa ufupi inatusaidia
kujijua sisi wenyewe na rafiki zetu. Dunia imekua mtaa na si kijiji
tena!
Facebook umebaki kuwa mtandao wenye watumiaji wengi zaidi kuliko mtandao wowote kwa mujibu wa takwimu za watumiaji mitandao za disemba 2012. Mpaka sasa mtandao huu wa kijamii una watumiaji zaidi ya Bilioni moja duniani kote!
Nchini Marekani imeonekana kuwa Facebook ni mtandao unaotembelewa zaidi kuliko mtandao uwao wote wa kijamii. Watumiaji milioni 152.2 wamekuwa wakitumia facebook kupitia kwenye kompyuta, milioni 152.7 wamekuwa wakitumia simu za mikononi.
Twitter, unabaki kuwa mtandao wa kijamii pekee ambao ni mshindani mkubwa wa Facebook. Ikiwa umeanzishwa miaka miwili baada ya mtandao wa facebook kuanzishwa, twitter sasa imejikusanyia watumiaji zaidi ya milioni 500 duniani kote. Mtandao huu umekua ukikua kwa kasi ya ajabu. umekua ni platfomu nzuri wa watumiaji wa blogs na mitandao mingi ya kijamii.
Taarifa zinaonyesha kwenye robo ya tatu ya mwaka 2012, twitter umekua ni mtandao pekee unaokua kwa kasi kuliko mitandao yote ya kijamii duniani. Mwaka 2009 twitter ilikadiriwa kuwa na watumiaji wapatao milioni 35.47 tu, lakini leo tayari ina watumiaji zaidi ya milioni 500.
Google+, kati ya mitandao ya kijamii ambayo kumekuwa na mkanganyo mkubwa kama kweli nao unagonga kwenye soko basi google plus ni mtandao ambao umezua zogo sana. Kiuhalisia si mtandao ambao watu wengi wanautembea sana lakini ni mtandao ambao umejizolea watumiaji milioni 400 sawa na mtandao wa kijamii wa Qzone wa China.
Hii ndiyo teknolojia yetu.
...........................................

No comments:
Post a Comment