Monday, September 16, 2013


KAMA ULIKUA HUJUI BASI HII NDO SABABU YA MAINDA KUPOTOE KATIKA FILAMU ZA BONGO MOVIE, SOMA HAPA



                                                    Cloud 112

MKALI wa sinema za Kibongo, Mussa Issa ‘Cloud 112’ amemchana mwigizaji Ruth Suka ‘Mainda’ kuwa stori nyingi za filamu nchini haziendani na Mainda na kudai ndiyo sababu za staa huyo kupotea. 
 Ruth Suka ‘Mainda’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Cloud 112 alisema maprodyuza wanashindwa kumchezesha Mainda katika ngazi muhimu kama ya mke kwani stori zinakuwa zinahitaji watu wenye umbo kubwa.
“Stori nyingi zinamkataa Mainda, mfano mimi siwezi kuigiza naye kama mke na mume kwani umbile lake na langu haliendani hivyo natoa wito kwa wasanii kumsaidia Mainda sababu ana uwezo mkubwa wa kuigiza,” alisema Cloud 112.

No comments:

Post a Comment