TAFITI INAONYESHA KUA VIBANDA VYA INTERNET VYAZIDI KUPOTEZA WATEJA
Kwa mujibu wa Utafiti wa huduma za Intaneti na Data Tanzania (2010) inaonyesha kuwa idadi ya watumiaji wa Intaneti kupitia vibanda imeshuka hadi kufikia asilimia 5.Miaka ya nyuma migahawa ya intaneti hususani katika miji mikubwa nchini ilitumika na watumiaji walio wengi zaidi.
Utafiti huo umeonyesha kuwa asilimia 55 ya watumiaji wa Intaneti wamekuwa wakitumia intaneti kupitia maofisini kwenye taasisi wanakofanyia kazi. Na asilimia 40 wamekuwa wakitumia huduma hizi kupitia majumbani au kwa simu za mikononi.
Utafiti huo umeonyesha kuwa ni asilimia 11 tu ya watanzania wote ndio wanaotumia huduma za Intaneti.
Kwa mujibu wa dodoso refu la Sensa ya Watu na Makazi 2012, kuna uwezekano idadi ya watumiaji wa Intaneti wakaongezeka zaidi nchini kwa kuwa kwenye Sensa hiyo kulikuwa na ukusanyaji wa takwimu za matumizi ya Intaneti kwenye kaya.
Mtandao mkubwa wa kijamii duniani (Facebook) umedhihirisha kwamba, 57% ya watumiaji wa facebook wamekuwa wakitumia huduma hiyo kwenye simu zao za mikononi. Mapinduzi ya Simu aina ya Smartphones pamoja na Tablets utabadilisha sana matumizi ya huduma za Intaneti nchini na hata kwingineko.
Hii inadhihirisha wazi kwamba migahawa ya Intaneti maarufu kama Internet Cafe itakufa nchini.
Unaweza kuisoma ripoti hii kupitia tovuti ya TCRA: (http://www.tcra.go.tz/publications/InternetDataSurveyScd.pdf)
Hii ndiyo Teknolojia Yetu.

No comments:
Post a Comment