TAZAMA KIFAA HIKI KINACHOFANYAKAZI KWA KUTUMIA SIMU ZA WINDOWS CHENYE UWEZO WA KUPIMA MARALIA NA KUTOA MAJIBU SAHIHI
Sanyansi
na teknolojia ndio vitu vinavyo run dunia kwa sasa, unaambiwa kutokana
na ugunduzi ambao Microsoft wenyewe wameutambua na kuwapa zawadi ya dola
za Kimarekani elfu kumi na mbili vijana waliofanikisha ugunduzi huo,
hivi sasa inawezekana kupima malaria bila hata kutoa damu lakini
hapohapo doctor wako akatumiwa taarifa za vipimo kwa njia ya electronic.
Kwenye mashindano ya Microsoft Imagine Cup kwa ajili ya vijana, vijana wanne kutoka Uganda wameweza kujishindia kiasi cha zaidi ya millioni 19 za kitanzania kwa kutengeneza Windows Application ambayo inafanya kazi na kifaa kingine kidogo cha nje ambacho mgonjwa anaweka kidole kama inavyoonekana kwenye picha ili application itoe majibu ya hali ya malaria mwilini.
Application hiyo waliyoipa jina la Matibabu kwa sasa inafanya kazi na windows phone lakini ili uweze kupima malaria unahitaji hiki kifaa cha nje.

No comments:
Post a Comment