Friday, September 27, 2013

                                  

                                            TAHADHARI TAHADHARI TAHADHARI  KWA WAKAZI WA IRINGA....................................kumeingia wizi mdogomdogo wa simu ambao unajitokeza katika manispaa ya iringa.....kijana mmoja anayefahamika kwa jina la DAVID LAWA amekua kidokozi wa simu za mikononi katika maofisi na sehemu mbalimbali anavyokua muonekano wake ni mtanashati vizur na mwisho wa siku anakuomba simu ampige na kusema anaacha  mizigo yake....na ukija kuangalia akiwa ameondoka unagundua ni mawe kwa hiyo kijana huyo anatafutwa na jeshi la polisi iringa kwa  msaada wa picha yake ni hiii hapa chini

                                         
KWA MSAADA PIGA NAMBA...........0767115584..................ASANTENI

TAFADHALI UKIPANDANDA BODABODA EPUKA SANA KUENDESHWA KWA MWENDO WA KASI, TAZAMA PICHA ZA AJALI MBAYA ILIYOTOKEA JANA MAENEO YA MANZESE MWEMBECHAI. {PICHA ZINATISHA}




WANANCHI WAKIANGALIA MWILI WA MAREHEMU


MWILI WA DEREVA BODABODA AJALI MBAYA SANA LEO IMESHUHUDIWA NA HABARI24 MAENEO YA MANZESE MWEMBECHAI AMBAPO DEREVA BODABODA AMEGONGWA VIBAYA NA KUFARIKI HAPO HAPO NA DALADALA








HII NDIO GARI ILIYOMGONGA DEREVA BODABODA MAENEO YA MANZESE

Tuesday, September 24, 2013

PICHA:KIGOGO WA TRA AMWAGIWA TINDIKALI,AWA KIPOFU..ALIA NA SERIKALI

*Sasa ni kipofu, adai serikali imemtelekeza Na Richard Konga, Arusha
TINDIKALI inaweza kuwa silaha hatari sana na haifai hata kidogo katika jamii, wanaokutwa nayo ingefaa wafungwe kifungo cha maisha kwani wanapoitumia vibaya huleta madhara yasiyoelezeka.

Elisha Kombe kabla na baada ya kumwagiwa tindikali.
Kuthibitisha hayo tunawaletea maelezo ya Elisha Kombe aliyekuwa Afisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Kitengo cha Upelelezi mkoani Mwanza, aliyemwagiwa tindikali akiwa katika majukumu ya kikazi mkoani humo.
Miaka 15 iliyopita alikuwa mchapakazi na tena mtanashati na nadhifu mwenye viungo kamili na alikuwa akifanya kazi yake kwa umakini mkubwa lakini leo, anaililia serikali kwa kile alichodai kumtelekeza baada ya kumwachisha kazi kutokana na tukio hilo lililomfanya awe kipofu.
Kombe alikutana na mwandishi wetu mwishoni mwa wiki iliyopita jijini Arusha ambapo anaishi na kaka yake, George Kombe baada ya kunusurika kifo kutokana na kumwagiwa tindikali wakati alipokuwa Mwanza kwa shughuli maalumu za kikazi.
Akisimulia mkasa huo wa kumwagiwa tindikali, Kombe alisema: “Nilipata uhamisho kutoka Makao Makuu ya Mamlaka ya Mapato Tanzania Dar es Saalam (TRA)  Septemba, 1997 kwenda mkoani Mwanza kwa ajili ya kazi maalumu ya ukaguzi na kudhibiti mianya ya ukwepaji wa mapato na magendo kwa baadhi ya wafanya biashara wasio waaminifu.
“Nikiwa Mwanza nilishuhudia mianya hiyo ya ukwepaji wa mapato kwa baadhi ya wafanya biashara waliokuwa wakitumia usafiri wa majini na baadhi ya meli na boti zilikuwa zikisafirisha bidhaa kwa njia isiyo halali sambamba na magari yaliyokuwa yakitumika nchi kavu.
“Pamoja na upinzani niliokuwa naupata vikiwemo vishawishi mbalimbali ili niweze kupunguza kasi ya utendaji niliokuwanao lakini nilikuwa na msimamo wa kutekeleza majukumu yangu ya kikazi kwa haki kama nilivyoagizwa na viongozi wangu,” alisema Kombe.

Aliongeza kuwa hali hiyo iliashiria kujengeka kwa hali ya chuki kwa baadhi ya mitandao ya wafanya biashara mkoani humo waliokuwa wakijishughulisha na biashara mbalimbali zikiwemo za mafuta, sabuni, bati na nyinginezo  huku wakibainika kukwepa kulipa mapato ya serikali.
Aliendelea kusema kuwa katika mamlaka hiyo aliitumikia zaidi ya miaka 11 akiwa ameitumikia serikali kwa uaminifu hadi Februari, 1998 alipomwagiwa tindikali na watu wasiojulikana wakati akigonga katika geti la nyumba aliyokuwa akiishi eneo la Kirumba jijini Mwanza.

ANAIKUMBUKA SIKU HIYO YA BALAA
“Ilikuwa ni majira ya saa nne ya usiku nikiwa katika hali ya matembezi ya kawaida ambapo katika matembezi hayo walijitokeza baadhi ya wafanyabiashara ambao walinisalimia ndipo baada ya kuachana nao nilielekea nyumbani kwangu, nilipofika kwenye geti nilianza kugonga ili mlinzi aje afungue ghafla niliitwa jina langu na mtu niliyehisi alikuwa nyuma yangu, nilipogeuka, ghafla nilimwagiwa tindikali kichwani,” alisema Kombe.
Akaongeza kuwa tukio hilo lililoashiria kupangwa lilimletea maumivu makali ya kichwa ambapo alipelekwa Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza na baadaye akahamishiwa KCMC. Baada ya kushindikana katika hospitali hizo alipelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Leeds iliyopo nchini Uingereza kwa ajili ya matibabu zaidi ambapo baada ya miezi minane alipata nafuu na kurudi nchini.
Kombe ameshangazwa na hatua ya serikali kumlipa shilingi milioni 12 kama mafao yake huku ikiwa imemtelekeza kwa kumwachisha kazi wakati ana familia ya watoto wanne  wanaomtegemea na kwamba fedha hizo hazimtoshi kutokana na majeraha aliyoyapata katika eneo la kichwa na maeneo mengine ya mwili wake.
“Naiomba serikali inipatie kazi kwani ulemavu wangu hauwezi kunizuia kufanya kazi katika idara yoyote au katika mamlaka hiyo hata kama ni kitengo cha huduma kwa wateja, mawasiliano na nyinginezo ili  niweze kujipatia kipato cha kuniwezesha kuishi na familia yangu na kunisaidia katika matibabu.”
Yeyote aliyeguswa na habari hii anaweza kumsaidia mpiganaji huyu wa uchumi wa nchi hii kwa simu namba 0787 926549 Kutoa ni moyo.

Monday, September 23, 2013

KAMA HUIJUI HISTORIA YA AL SHABAAB BASI KARIBU UISOME HAPA UJE WALITOKEA WAPI HADI LEO WAMEKUA TISHIO

Kundi la wapiganaji wa kisomali la al-Shabaab,limevamia jumba la kifahari lenye maduka na mikahawa nchini Kenya. Al Shabaab lenya mizizi yake nchini Somalia, limeweza kuondolewa kutoka miji mikubwa ya Somalia ikiwemo Mogadishu na sehemu zengine za Somalia , ingawa bado linasalia kuwa tisho kubwa kwa kanda nzima.

Al Shabaab ni nani?

Jina Al-Shabab linamaanisha Kijana kwa lugha ya kiarabu. Kundi hilo liliibuka kama tawi la vijana la muungano wa mahakama za kiislmau ambao baadaye ulivunjika mwaka 2006, wakati ilipopigana na wanajeshi wa Ethiopia waliokuwa wameingia nchini Somalia kuunga mkono serikali iliyokuwa dhaifu.
Kuna taarifa chungu nzima kuhusu wapiganaji wa kiisilamu wanaokwenda Somalia kupigania Al Shabaab.
Kundi hilo limeweka sheria kali za kiisilamu katika maeneo ambayo linadhibiti ikiwemo kupigwa kwa mawe hadi kufa wanawake wanaodaiwa kufanya uasherati pamoja na kuwakata wezi mikono.

Je Al Shabaab linadhibiti sehemu gani ya Somalia?

Ingawa kundi hilo limepoteza udhibiti, wa miji mikubwa, bado linakita mizizi katika maeneo ya mashinani.
Lililazimika kuondoka katika mji mkuu Mogadishu, mwezi Agosti mwaka 2011 na pia kuondoka katika mji wa bandarini wa Kismayo mwezi Septemba mwaka 2012.
Kismayo ulikuwa mji muhimu kwa kundi hilo, ambao ulikuwa unawezesha bidhaa kuwafikia wapiganaji wa kundi hilo pamoja na kuwatoza watu ushuru kwa shughuli zao.
Hizi ni silaha za Al Shabaab walizonasa wanajeshi wa AU
Muungano wa Afrika, ambao unaunga mkono juhudi za majeshi ya serikali, ulisherehekea ushindi huo ingawa al-Shabab hunfanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kujitoa mhanga mjini Mogadishu na kwingineko.
Wadadisi wanaamini kuwa al-Shabab limeanza kufanya mashambulizi ya kuvizia baada ya kushindwa na majeshi ya Muungano wa Afrika wanaotumia nguvu dhidi yao.
Lakini linakabiliwa na tisho kubwa kutoka kwa wanajeshi wa Kenya walianza hatarakti zao dhidi ya kundi hilo kuanzia mwaka 2011.
Kenya ilituhumu wapiganaji wa al-Shabab kwa kuwateka nyara wanajeshi wake pamoja na watalii na sasa wamekuwa katika msitari wa mbele kupambana na kundi hilo la kigaidi.
Wakati huo, wanajeshi wa Ethiopia waliweza kukabiliana na wapiganaji hao na kudhibiti miji ya Beledweyne na Baidoa.

Nani kiongozi wa al-Shabab?

Ahmed Abdi Godane ndiye kiongozi wa kundi hilo. Anajulikana kama Mukhtar Abu Zubair, na anatoka katika jimbo la Somaliland.
Kumekuwa na taarifa za mgawanyiko katika kundi hilo, ambazo hata hivyo zinapingwa vikali na kundi lenyewe. Inaarifiwa kuwa uongozi wake unapingwa, na wanachama wanaotoka maeneo ya Kusini na ambao ni wengi katika kundi hilo. Inakisiwa idadi yao ni kati ya wanajeshi 7,000 na 9,000.
Bwana Godane huwa haonekani hadharani . Mtangulizi wake Moalim Aden Hashi Ayro, aliuawa katika shambulizi lililofanywa na Marekani mwaka 2008.

Nini uhusiano wa kimataifa wa kundi hilo?

Al Shabaab wakifanya mashambulizi mjini Mogadishu
Al-Shabab lilijiunga na al-Qaeda mwezi Februari mwaka 2012. Katika ujumbe wa Video, kiongozi wa al-Shabab Ahmed Abdi Godane alisema anaahidi kuunga mkono kingozi wa al-Qaeda Ayman al-Zawahiri.
Makundi hayo mawili yamekuwa yakifanya kazi kwa pamoja, na raia wa kigeni wamekuwa wakiunga mkono kundi hilo, na hata kuwasaidia katika harakati zao za mapigano.
Mwaka jana maafisa wa al-Shabab waliambatana na mtu aliyesema ni mwanachama wa al-Qaeda na kumtambua kuwa raia wa Marekani Abu Abdulla Almuhajir alipokuwa anatoa msaada wa chakula kwa waathiriwa wa njaa.
Maafisa nchini Marekani wanaamini kuwa wapiganaji wa Al Qaeeda ambao hawajahusina sana na mashambulizi nchini Afghanistan na Pakistan kufuatia mauaji ya kiongozi wao,Osama bin Laden, wapiganaji wake wengi wanakwenda kutafuta hifadhi nchini Somalia

TAZAMA PICHA ZA SIMBA ALIE SUMBUA NA KUUWA MIFUGO MJINI MOROGORO BAADA YA KUULIWA..!!

Kwa kimombo tunaiita 'life and death', Simba aliyetumia fursa vizuri kwa kujilia mbuzi 47 ameyaonja mauti baada ya kupigwa hadi kufa na Askari wanyamapri.
Simba huyo ambaye amesumbua kwa muda mrefu Mkoani humo maaskari Wanyamapori Mkoani Morogoro wamemwinda na kumuua simba huyo aliyetafuna mbuzi 47 katika Mlima Uluguru eneo la kijiji cha Bagilo kata ya Kinole, Tarafa ya Mkuyuni Mkoani humo.



Askari wanyamapori Wakimchuna ngozi simba

SAMAHANI PICHA HII INATISHA;AJALI MBAYA YAMKUTA MWENDESHA PIKIPIKI MAARUFU KAMA ASSECDO NI MITAA YA MIEMBENI BUKOBA

Ajali mbaya yamkuta mwendesha pikipiki mjini bukoba maarufu kama Assecdo, na kupuata madhara ya majeraha makubwa kichwani na mkononi kama inavyo onekana katika picha.
Ni baada ya kupalamia ukuta wa duka la nyama lililopo mitaa ya miembeni Center usawa wa kutokea barabara ya bukoba sekondari
Mpaka anapelekwe hospital hali yake haikuwa nzuri,ni tukio la mchana wa jumamosi weekend hii.
hadi tunaingia mitamboni atujapata habari zaidi kuhusiana na tukio hili na ukweli ni kwamba hali ya biashara ni tete ndani ya Burchar hiyo .
Picha kwa hisani ya Mdau Jon Do Pesa na Bukoba wadau blog

PICHA YA KWANZA YA MSEMAJI WA AL-SHABAAAB AKIJIGAMBA KWA KUWAUA WANANCHI WA KENYA JANA AT THE MALL!!

Al-Shabab spokesperson Ali Mohamud Rage holds a news conference in Mogadishu, Somalia.