-
Habari ya kweli iliyotokea wiki iliyopita.
Kuna
dada mmoja anasoma chuo buguruni na pia ni mfanyakazi hivyo jioni
akitoka kazini ndipo huenda shule.Sasa akiwa njiani kuelekea chuo
akapigiwa simu na mtu asiyemfahamu akajitambulisha kwamba yeye ni
daktari wa lugaro hosp na kumuulizia habari za mwanae ambae alishawahi
kwenda kumtibu pale na chakushangaza zaidi akataja mpaka aina na rangi
ya nguo aliyovaa siku ile alipokwenda hapo hospitali na yote yalikuwa
kweli.
Na zaidi akamwambia najua sasa hivi unaelekea chuo buguruni na
kweli ilikuwa hivyo, lakini mwishoni akamweleza kwamba kuna mambo
anataka kujua kujua kuhusu hicho chuo hivyo nae anaelekea huko hivyo
akifika tu atamtafuta. Kwa muda wote huo huyo dada hakuweza kabisa
kumkumbuka ila akajipa moyo kwamba yamkini huyo mtu atakuwa anamfahamu
vizuri.
Baada
ya kutoka chuo akiwa na wenzake watatu akawa anawasimulia habari za
huyo mtu ndipo simu yake ikaita,kupokea yule mtu akamwambia nakuona uko
na wenzio wawili mnavuka barabara na kumueleza jinsi alivyovaa sasa
wenzie wakasema huyo mtu anakufahamu haiwezekani hapa tupo watatu kweli
na ameweza kukutambua. Kisha huyo mtu akamwelekeza mahali alipo ambapo
haikuwa mbali na barabara.
Lakini
alipomtazama hakumfahamu kabisa, basi akampa mkono kumsalimia, baada ya
hapo hakujitambua na zaidi alijikuta yuko maeneo ya chuo kikuu cha DSM
akiwa hoi. Kuangalia simu na kila kitu chake kilikuwa salama na
hakufanyiwa kitu chochote, kwa bahati kulikuwa kuna ndugu yake anasoma
chuo hivyo akawasiliana nae ili kupata msaada ikabidi awahishwe
mwananyamala hosp lakini ikaonekana sumu iliyotumika ni kali na dawa
yake wanayo regency hosp,hivyo akawahishwa regency na kupata matibabu.
Baada
ya ufahamu kumrudia akakuta mtu huyo kachukua pesa zote kwenye
mpesa,tigo pesa na bank ( NMB na CRDB) kiasi cha milioni 3, hivyo
inawezekana walipompa sumu alitaja password pasipo kujijua.
Na
bank walipotazama kwenye ATM Camera waliona picha ya huyo mtu na yeye
alimkumbuka vizuri, lakini polisi Kijitonyama wakakiri kwamba kesi hizo
sasa hivi zimetokea mara nyingi na huo mtandao ni mkubwa, walipoenda
kwenye usajili wa simu walikuta ni huyo huyo na jina lake ndilo
alilojitambulisha.Ingawa polisi wameshindwa kumkamata.
Akiwa
kituo cha polisi mara huyo mtu akampigia simu akimwambia ‘’kumbe wewe
ni muoga sana tutakurudishia pesa zako’’. Sasa kumbe wanachofanya
wanakuambia’’ tutafutie mtu ambae unahisi ana pesa kuliko hizi halafu
tukifanikiwa tutarudisha pesa zako’’ hivyo inawezekana nae kuna mtu
anaemjua alifanyiwa hivyo akaamua kumtaja yeye