Thursday, January 31, 2013

BREAKING NEWS......MOTO WATEKETEZA KIWANDA CHA CHEMI COTEX DAR

Moto mkubwa umezuka na unakiunguza kiwanda cha vipodozi cha ChemiCotex kilichopo huko Africana njia ya Tegeta jijini Dar es Salaam.

Chanzo cha moto huo hakijafahamika ingawaje inahisiwa kuwa huenda ni hitilafu iliyotokana na fundi aliyekuwa akichomelea kitu ndani ya kiwanda hicho.

Wahusika wakuu wa kiwanda hicho hawakuwa katika eneo husika ili kutoa maelezo zaidi. Taarifa zinasema kuwa magari ya kikosi cha zima-moto yalipowasili, watu walianza kuyarushia mawe kiasi cha kutishia usalama wa watu wengine ambao waliamua kuondoka kutoka katika eneo la tukio.

Jitihada  za  kumtafuta kamanda  wa  polisi  wa  kanda maalum ya Dar es Salaam Suelein Kova  bado zinaendelea baada ya simu yake  kuita bila  kupokelewa .(picha na wavuti)

Wednesday, January 30, 2013

RAIS JOSEPH KABILA WA DRC ATUA DAR LEO KWA ZIARA YA SIKU MOJA


 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimjpokea Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimtambulisha maafisa mbalimbali Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam mchana wa leo Januari 30, 2013


  Rais Jakaya Mrisho Kikwete na mgteni wake  Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakmiangalia ngoma za utamaduni alipowasili uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere jijijni Dar es salaam  mchana wa leo Januari 30, 2013
Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Joseph Kabila wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wakiingia hoteli ya Hyatt  Kilimanjaro jijini mchana wa leo Januari 30, 2013
PICHA NA IKULU

WASANII IRINGA WATOA USHAURI WA BURE KWA LULU WATAKA AOKOKE



Wapenzi  wa  muziki  filam mkoani Iringa  wametoa onyo kwa msanii Elizabeth Michael maarufu Lulu aliyetoka kwa  dhamana  mahabusu kufuati  tuhuma ya kesi yake ya mauwaji ya msanii mwezake Stivin Kanumba ,kuwa anapaswa  kutumia muda huu kuwa  jirani ni kanisa badala ya  kupenda starehe za dunia.

Wakizungumza na mtandao huu  wa  www.francisgodwin.blogspot.com wasanii hao Johari John na Kevin Sanga  walisema  kuwa dhamana ya Lulu ni mapenzi ya Mungu  hivyo mbali ya  kutoka mahabusu kwa dhamana bado anapaswa  kuishi kwa utulivu zaidi muda  wote ikibidi kuanza  kuwa karibu na kanisa.

Hata  hivyo John alitaka  waumini wa madhehebu mbali mbali kuendelea  kumwombea msanii  huyo ili Mungu aendelee  kusimama upande  wake.

Wasanii hao  walisema  kuwa  suala la msanii  huyo  kuendekeza  kujirusha kwa  sasa asilipe nafasi katika maisha yake na badala yake  kumgeukia Mungu  zaidi na kuachana na mambo ambayo hayampendezi mwenyezi Mungu.

MTUHUMIWA WA MAUWAJI YA MWANGOSI KUFIKISHWA TENA MAHAKAMANI KESHO

Huyu ndie mtuhumiwa wa mauwaji ya Daudi Mwangosi
MTUHUMIWA  wa  mauwaji ya aliyekuwa mwandishi wa habari wa kituo cha Chanel Ten mkoani Iringa marehemu Daudi Mwangosi askari  wa FFU mwenye namba G2573 Pasificus Cleophace Simoni (23)ambae  alishindwa kufikishwa mahakamani katika kesi yake  baada ya kudaiwa kuwa ni mgonjwa sasa atafikishwa  tena mahakamani kesho Januari 31.
Kesi   hiyo ambayo ilitajwa Januari 27 ambapo mtuhumiwa huyo hakuweza kufikishwa  mahakamani  hapo baada ya mahakama  hiyo  kuelezwa  kuwa mtuhumiwa   huyo ni mgonjwa na  imeshindikana  kufikishwa mahakamani hapo.
 
Mwendesha mashtaka  wa jamhuri Adolf Maganda aliieleza hakimu  wa mahakamani ya hakimu mkazi  wilaya ya Iringa Dyness Lyimo kuwa mtuhumiwa alipaswa  kufikishwa mahakamani hapo  Januari 27  ila ilishindikana  kutoka na taarifa  kuwa ni mgonjwa  hivyo  kuomba  kupangwa  tarehe nyingine ya kutajwa  kesi hiyo ambayo  bado  upelelezi wake  kukamilika .
Hata  hivyo mahakamani  hiyo  liahirisha  kesi hiyo  hadi  kesho Januari 31  itakapotajwa  tena .
Mtuhumiwa  huyo anatuhumiwa  kumuua kwa makusudi kwa   bomu aliyekuwa  mwandishi  wa habari wa Chanel Tena  mkoa  wa Iringa  marehemu Mwangosi  septemba 2 Septemba mwaka jana  katika kijiji cha Nyololo Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa  wakati  wa vurugu kati ya  polisi na wafuasi wa  Chadema .kinyume na kifungu cha sheria namba 148 kifungu kidogo 5A.i cha makosa ya jinai. Kwa mujibu wa kesi za jinai, sheria kifungu 196 kanuni ya adhabu Cap. 16 iliyofanyiwa marejeo mwaka 2002,

Monday, January 28, 2013

http://snd.sc/XOqy35

UPDATES:LULU MPAKA SASA HAJATIMIZA MASHARTI YA DHAMANA

Kwa habari ambazo zimetufikia ni kwamba baada ya Lulu kupata dhamana yake ya kuachiwa,lakini mpaka sasa ni kwamba hajaachiwa kwasababu ya taratibu za dhamana hazijakamilika.
 ili atoke inabidi masharti na taratibu za mahakama zifuatwe na ndipo kusainiwa na Msajili wa Mahakama Kuu.
Kwa leo asipoachiwa huenda akarudi tena segerea kutokana na taratibu hizo za mahakama ila kesho hatapelekwa tena Mahakamani kwa kusikiliza Dhamana yake.

RICKY ROSS ANUSURIKA KIFO BAADA YA KURUSHIWA RISASI

 Msanii Ricky Ross, leo asubuhi amenusurika kifo baada ya mtu mmoja aliekua na silaha kurusha risasi kadhaa kwenye gari aina ya Rolls Roys aliyokuwemo Ross na dem mmoja Ft. Lauderdale, Florida na kusababisha kugonga nyumba akijaribu kuongeza mwendo.
Ross hakupatwa na risasi hata moja wakati wa tukio hilo wala dem aliekuwa nae ndani ya gari hilo.
Ripoti zinadai risasi kibao zilirushwa kuelekea kwenye gari hilo mda wa saa kumi na moja asubuhi, na hakuna hata moja iliyoshoot kwenye Rolls.
polisi wanasema gari lingine lilisimama karibu na gari la Ross na mtu mmoja aliekuwa kwenye gari hilo kuanza kurusha risasi kwenye gari la Ross
 Mpaka sasa hakuna alietuhumiwa, kugundulika wala kushikiliwa juu ya tukio hilo


TEJA AKUTWA AMEKUFA KWA KUJIDUNGA MADAWA YA KULEVYA

Nyumba ambayo mwili  huo umekutwa
mwili  wa kijana Stan Mhepelwa ukiwa katika gari ya polisi leo
Bomba la sindano lililokutwa katika chumba  hicho
Mwili  wa kijana  huyo ukitolewa

Kijana anayesadikika kuwa mtumiaji  wa madawa ya  kulevya (teja) mjini Iringa Stan Mhepelwa  mkazi  wa Ilala katika Manispaa ya Iringa amekutwa akiwa amekufa katika  nyumba  ambayo bado  kukamilika eneo la barabara  mbili katika Manispaa ya Iringa.

Mashuhuda wa  tukio  hilo  wameueleza mtandao  huu wa www.francisgodwin.blogspot.com  kuwa  tukio  hilo  limetokea  usiku  wa kuamkia leo  jumapili ambapo  mwili  wa  kijana  huyo  umekutwa  mida ya saa 3 asubuhi  na  wananchi  waliokuwa  wakipita  eneo  hilo .

Samson Kalinga ni mkazi  wa  eneo  hilo amesema  kuwa  nyumba  hiyo imekuwa  ikitumiwa na vijana hao mateja kama  sehemu ya  kujificha na kujidunga madawa  ya  kulevya kwa  kutumia sindano na kuwa  chanzo  cha kifo cha kijana  huyo kinasadikika kuwa alijidunga sindano  vibaya .

Hata  hivyo  alisema mwili  wa  kijana huyo umekutwa katika  chumba  hicho huku pembeni  kukiwa na mabomba ya sindano na kuwa aliyetoa siri ya  kifo cha kijana  huyo ni teja mwenzake ambae  alikuwa akiingia katika  chumba  hicho ili kuendelea  kutumia madawa  ya kulevya.

MAHAFALI YA KIDATO CHA 6 YAFANA

wanafunzi wa kidato cha 6 lugalo wakisoma risala.

wanafunzi wa kidato cha 6 wa shule sekondari Iringa wakicheza kwaito wakati wa mahafali yaliyofanyika shuleni hapo mwishoni mwa wiki. picha na denis mlowe

UTULIVU WAREJEA MTWARA WANAJESHI WAINGIA MITAANI , ZAIDI YA 40 WAKAMATWA , WAZIRI MKUU ATUA KUOKOA JAHAZI

watuhumiwa wa vurugu wakikamatwa

Hali ya  utulivu  inadaiwa  kurejea katika wilaya ya Masasi  mkoani Mtwara baada ya   vikosi  vya jeshi la wananchi Tanzania (JWTZ) na  polisi  kuungana  kuweka ulinzi huku  watu  zaidi ya 40  wakikamatwa  kuhusika na matukio  ya vurugu za jana.

Mwandishi  wa mtandao  huu  kutoka Mtwara John Kasembe anaripoti  kuwa kutokana na vurugu  hizo  waziri mkuu Mizengo Pinda na  waziri wa mambo ya ndani Dk Emmanuel Nchimbi usiku  huu wapo Mtwara  wakiendelea na vikao  vya  kurejesha amani na utulivu mkoani hapo.

Pia inadaiwa  mida ya asubuhi  leo  polisi  walilazimika  kutumia mabomu ya machozi  kuwatawanya  vijana ambao  walikuwa  wamefunga barabara na  kuwatoza ushuru  batili  wa shilingi 5000 wenye magari kama sehemu ya kujipatia fedha kwa njia feki.

Mbali ya tukio  hilo bado katika mitaa mbali mbali ya Mtwara  kwa siku ya leo shughuli  zote za uzalishaji mali zikiwemo biashara zimesimamishwa kwa  muda  ili  kukwepa vurugu kama za jana  japo shughuli za ibada  zimeendelea kwa  utulivu  zaidi.

HEMED PHD NDANI YA "TOP 20 COUNTDOWN" YA CHOICE FM LEO JIONI


Kama wewe ni shabiki wa Hemed Phd basi leo hupaswi kukosa kumsikiliza akitangaza kipindi cha The Countdown cha nyimbo 20 kupitia Choice Fm ya Dar es Salaam.

Kipindi hicho huruka kuanzia saa tisa mchana mpaka saa kumi na moja jioni.Choice Fm husikika Dar es Salaam pekee kupitia 102.5 FM na kwa njia ya internet.

HUYU NDO STAR WA HIGH SCHOOL MUSICAL STAR, ALIYEAMUA KUWASHTAKI WAZAZI WAKE KWA KUMWIBIA HELA ZAKE

0125_chris_warren_jrAs if his famous mom's divorce wasn't bad enough -- "High School Musical" star Chris Warren has now filed a lawsuit against BOTH his parents, accusing the pair of stealing hundreds of thousands of dollars of his child acting money.

Warren filed the lawsuit against "Passions" actress Brook Kerr and Christopher Warren Sr., claiming they established a trust for him back in 2001 for all the money he made as a minor -- and have been secretly dipping into the kitty ... big time.

0125_subasset_chris_warren_jr
According to the lawsuit, Chris paid into the account for years, but when he decided to make a withdrawal back in 2011 -- as a 21-year-old -- his parents refused to grant him access.

When pressed, Chris claims his parents admitted they had blown through hundreds of thousands of dollars of his money on their own personal expenses ... but refused to say how much was left in the account.

Chris is now suing his parents for all the money back ... even though he's still not sure exactly how much they took.

Reminder: Chris' parents are currently embroiled in a nasty divorce.

Neither parent has responded to Chris' lawsuit.

CHECK OUT PICHA ZA MACHANGUDOA WAKIPELEKWA MAHAKAMANI....

 
Wanawake wanaotuhumiwa kufanya biashara ya ukahaba wakiwa Chini ya Ulinzi wa askari kwenye Mahakama ya Jiji la Dar es Salaam, baada ya kukamatwa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kinondoni kwenye oparesheni ya kuwakamata inayofanywa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Kipilisi Kinondoni, jumla ya watuhumiwa 14 pamoja na baadhi ya wateja wao wamefikishwa kwenye mahakama hiyo.


Wanawake hao wakiwa na baadhi ya wateja waliokutwanao wakifanya ngono baadhi yao wakificha sura zao.

Wakiwasili kwenye mahakama ya jiji huku wakificha sura ili wasionekane.

Sunday, January 27, 2013

OMMY DIMPOZ NA VANESSA MDEE WAENDA KENYA KUSHOOT VIDEO YA ME & YOU

Ommy Dimpoz na Vanessa Mdee wakisindikizwa na AY, jana wamewasili salama jijini Nairobi Kenya ambako wameenda kushoot video ya Me and You.
Video hiyo inafanywa na kampuni ya Ogopa Dj’s ambayo hivi karibuni ilishoot video ya Diamond, Kesho. Me and You ni single ya tatu ya Ommy yenye mafanikio makubwa.

PICHA 20 ZA MAANDAMANO YA JANA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA ST. JOHN, WALIPOANDAMANA KULALAMIKIA UBAKAJI NA MAUAJI CHUONI HAPO

Huyu jamaa alielala chini ni mtuhumiwa aliekamatwa asubuhi ya leo, ambapo wanafunzi walivamiwa na kuibiwa Laptop kisha wavamizi hao kuchoropoka. Wanafunzi ilibidi wajikusanye muda huo huo na kuwasaka ndipo walipokutana na jamaa huyo ambae alikuwa haeleweki na baadae ikafahamika ni mmoja wao

Basi mtuhumiwa huyo alichukuliwa na polisi kisha wanafunzi waliingia chuoni kuanzisha maandamano

Hapa walikusanyika kwenye bendera kisha kuongea na mkuu wa chuo

Mkuu wa chuo alisema pia nao wamechoshwa na mambo mabaya ambayo wanafunzi wanafanyiwa. Hivyo wanafunzi wawe na subira wanafanya taratibu za kibari cha maandamano ya amani

Wanafunzi baada ya kusubili kwa muda mrefu kibari icho wakaamua kuandaa mabango kwa ajili ya maandamano, ambapo kibari kipatikane kisipatikane walidai kuandamana ni lazima
Basi wanafunzi wakaanza kuchora mabango yao kwa ajili ya maandamano



Mabango yalipokamilika wakasimama kwenye bendera kwa mara nyingine



Walifika mbali na kuona kuwa polisi wanahusika katika mambo mabaya wanayofanyiwa. Ndipo wakachora bango hili kuonyesha hisia zao
Wakaamua kuingia barabarani kwa maandamano baada ya kujaa munkari na jaziba kubwa
Hapa wapo barabarani na masomo kwa siku ya leo hayakuwepo

Bango lina picha ya mwanafunzi alieuliwa kikatili, aliefahamika kwa jina la LYDIA LEO






Ni mchaka mchaka ulioendana na nyimbo za hisia

Magari yalisimama kwa muda mrefu mjini hapo mpaka wanafunzi walipomalizika kupita, kwa hiyo wenye haraka walichelewa

Haya huyu anaashiria demokrasia na maendelea ndio imetawala juu yao

Msafara hapa unaelekea maeneo ya Bungeni

Kila walipopita walikuwa wakishindikizwa na polisi kuhakikisha amani inatawala

Hakuna kitu ambacho kiliniacha hoi baada ya wanafunzi kwenda mpaka Bungeni, kisha walipofika wakaimba nyimbo ya Taifa. Polisi waliwaomba kuongea na viongozi wa maandamano hayo wakajibiwa na wanafunzi kuwa kiongozi wao hameishakufa ambae ni mama LYDIA LEO

Gari la maji ya kuwasha lilikuwepo lakini wanafunzi hao hawakutishika na kitu chochote kile kutoka kwa Polisi



Wanafunzi walifika mpaka Nyerere Square waliimba nyimbo mbalimbali mahala hapo




Baada ya kutembea mji mzima na mabango yao na kuhakikisha kiu yao imekwisha basi waliamua kurudi chuoni

Gari la washa washa nalo lilikuwepo lakini watu walikuwa na jaziba zao vilevile mwanzo mwisho
Barabara zilikuwa zimetawaliwa na wanafunzi kwa kiasi kikubwa, mpaka kusababisha magari kutopita

Hapa ilibidi nipande gari la polisi ili niweze kuchukua picha vizuri, sio siri polisi wenyewe walikuwa wamechoka kwa kutembezwa mji mzima baada kuchat nao kwenye gari ilo

Hapa ndipo safari ya maandamano ilipoanzia na ndipo safari hiyo ilipoishia maeneo haya ya kwenye bendera mbele ya jengo la administration.