Wednesday, February 13, 2013

BREAKING NEWS....NYUMBA YATEKETEA KWA MOTO WA KIMIUJIZA IRINGA

 Mkazi  wa Zizi la Ng'ombe kata ya Isakalilo mjini Iringa Juma Said ( kushoto) akiwa na askari  wa jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Iringa na askari wa  upelelezi  wakitazama vifaa vyake vya muziki ambavyo  zimeteketea kwa  moto  mchana wa  leo
 Askari  wa Zimamoto na wakikusanya mabaki ya mali  za  mkazi huyo baada ya  kuteketea kwa  moto
 Askari  wa  jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa  wa Iringa (kulia)  wakimshauri mkazi  wa Zizi la Ng'ombe kata ya Isakalilo mjini Iringa Juma  said kushoto kutoa nje ya nyumba mali zake zote  zilizoteketea kwa moto ili kuzima  kuhakiki moto zaidi
 
 Wananchi  wa Isakalilo wakitazama nyumba ambayo ilikuwa ikiteketea kwa moto  kimiujiza
 Mali  zilizoteketea kwa moto
 Magari  ya  Zimamoto yakiwa kazini leo
 Magari ya  Zimamoto na lile la jeshi la polisi wakiwa katika  eneo la tukio
 Mali  zilizoteketea moto  leo




 Bw Juma  Said akikusanya mabaki ya mali zilizosalia katika tukio  hilo la moto

MOTO mkubwa  uliowaka kimiujiza  umetetekeza  nyumba na mali  mali mbali mbali zilizokuwemo katika nyumba ya mkazi  wa mtaa wa  Izizi la Ng'ombe kata ya Isakalilo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Bw .Juma Said.

Tukio hilo  limetokea  leo majira ya saa 6.38 mchana  wakati mmiliki  wa  nyumba  hiyo akiwa katika  shughuli nyingine za kikazi mbali na eneo  hilo la Zizi la Ng'ombe.

Wakizungumza na mwandishi  wa mtandao  huu  wa www.francisgodwin.blogspot.com eneo la tukio baadhi ya mashuhuda  walisema  kuwa  wameshangazwa  kuona moto mkubwa  ukiwaka katika paa la nyumba  hiyo  ambayo  ilikuwa haina mtu yeyote.

Alisema mmoja kati ya mashuhuda  Sarah Sanga  kuwa baada ya  kuona moto ukiwaka juu ya paa la nyumba  walilazimika  kufika  eneo hilo na kutaka  kujua kama moto  huo  unatoka katika nyumba hiyo ama ni nyasi  zimechomwa  jirani na  nyumba  hiyo.

Hata  hivyo  alisema baada ya  kufika jirani na nyumbani hiyo ndipo  walipobaini  kuwa katika  nyumba  hiyo hakukuwa na mtu na milango yote  ilikuwa  imefungwa na ndipo  walipoamua  kuanza kuzima moto  huo kwa  kumwagia maji huku baadhi yao  wakiwasiliana na  jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa  wa Iringa ambao  walifika haraka eneo  hilo na kufanikiwa  kuvunja milango ya nyumba hiyo na kuzima moto mkubwa ambao tayari  ulikuwa  umeshika kasi zaidi.

Ally Omary alisema  kuwa  hakuna  mwananchi ambae  anatambua  chanzo  cha moto  huo  kutokana na nyumba hiyo  haikuwa na umeme  wa Tanesco  zaidi ya umeme  wa genereta ambalo pia  lilikuwa  limezimwa.

"Tunapenda  kuwapongeza sana  hawa  watu  wa zimamoto Iringa kwa  kufika haraka  zaidi  tena  wakiwa na magari  mawili na kusaidia kuzima moto  huo vinginevyo madhara  ambayo  yangejitokeza yawezekana yangekuwa makubwa  zaidi ikiwa ni pamoja na nyumba  za jirani  kushika moto"


Mmiliki wa nyumba  hiyo Juma Said alisema  kuwa  moto  huo ulianzia chumbani  kwake ambako  kulikuwa na mali mbali mbali  vikiwemo  vyombo  vya muziki na mali nyingine  nyingi ambazo  zote  zimeteketea  .

Said  alisema  kuwa moto  huo unaonyesha umeanzia  kuwaka katika radio kutokana na jinsi ambazo mazingira  yanaonyesha na kuwa hadi  sasa thamani  ya mali  zote  na uharibifu uliojitokeza bado  kufahamika.

" Kweli nashindwa kujua  moto  huu ndani ya radio umeingiaje kwani ninavyoondoka radio ilikuwa haifanyi kazi na nyumba haina  umeme zaidi ya Genereta ambayo  huwa inawashwa  usiku"

Diwani  wa kata   ya Isakalilo  Bernad  Kanika alisema mmiliki wa  nyumba hiyo  ambae amejeruhiwa kutokana na jitihada za kuvunja vioo  kwa mikono amepelekwa  kutibiwa huku akidai kuwa chanzo cha moto  huo bado hakifahamiki kutokana na mazingira  yanavyoonyesha.

Mkuu  wa  kituo cha jeshi la Zimamoto na uokoaji mkoa wa Iringa John Chadewa  alithibitisha  kutokea  kwa  tukio  hilo na kuwa  jitihada zao na zile za  wananchi  wa  eneo hilo zimeweza  kusaidia  kuzima moto  huo huku akisema changamoto  kubwa ni ujenzi  holela ambao wananchi  wamekuwa  wakijenga hadi katika barabara  na kukwamisha gari ya  zimamoto  kupita kwa urahisi zaidi.

No comments:

Post a Comment