Tuesday, February 5, 2013

HILI NDO JUMBA LA KIFAHARI LA MICHAEL JORDAN, NI BONGE LA JUMBA LA KISASA

Baada ya miaka miwili ya mipango na ujenzi, hatimaye jumba la kifahari la mcheza kikapu mwenye mafanikio na jina kubwa kutoka marekani, Michael Jordan limekamilika. Mansion hiyo iliyojengwa South Florida imekamilika ikiwa na thamani ya dola za kimarekani 12.4 milioni.
Ona picha zaidi za Mansion hiyo:
Michael Jordan ni mcheza kikapu wa siku nyingi katika ligi ya NBA nchini Marekani, baadhi ya timu alizowahi kuchezea ni Chicago Bulls na Cleveland Cavaliers. Kwa sasa MJ ni mjasiriamali akimiliki hisa nyingi na pia ni mwenyekiti wa timu ya mpira huo ya Charlotte Bobcats.
Michael anatajwa na website ya NBA kuwa ni mcheza kikapu mkubwa ambae hajawahi kutokea, yaani "Greatest basketball player of all time"
CHANZO GongaMx News Team.

No comments:

Post a Comment