PICHA 15 ZIKIONYESHA MELI YA MV VICTORIA AKIWAKA MOTO, NA HARAKATI ZA KUUZIMA MOTO HUO
![]() |
MELI
ya Mv Victoria inayomilikiwa na Kampuni ya huduma za Meli nchini (MSC)
imenusurika kuteketea kwa moto uliozuka wakati mafundi wa kampuni hiyo
wakichomelea eneo la shimo la kuhifadhia mizigo la mojawapo ya maeneo
kwenye Meli hiyo.
Moto huo uliozuka katika meli hiyo ulizua tafrani kwa wakazi wa jiji
la Mwanza na kufurika katika eneo la maegesho ya Meli za Kampuni ya MSC
yaliyopo katika bandari ya Mwanza kaskazini majira ya saa 8 na dakika
kadhaa na kusababisha msongamano mkubwa katika eneo hilo.
|
![]() |
Kwa mujibu wa taarifa zilizo naswa toka kwa wafanyakazi wa Meli hiyo
ambao hawakutoa ushirikiano kuzungumza na waandishi wa habari,
zilizonaswa wakati wakilaumiana zimeleeza kuwa mafundi wa kampuni hiyo
walikuwa wakichomelea katika moja ya vyumba vya chini vya Meli hiyo
ndipo cheche za moto zilipopenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya
kuhifadhia mizigo na kuanza kuwaka.
Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa shehena ya magodoro
pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini
Bukoba Mkoani Kagera leo usiku.
|
![]() |
| Ni hali halisi ndani ya Sehemu hiyo ya mizigo kulikuwa kumehifadhiwa magodoro pamoja na mito ya makochi tayari kwa ajili ya kusafirishwa kwenda mjini Bukoba Mkoani Kagera leo usiku. |
![]() |
| Maafisa wa kikosi hicho walijitosa kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria ambapo walifanikiwa kuuzima huku ukiwa tayari umeteketeza magodoro yote pamoja na mito ya makochi iliyokuwa katika chumba cha kuhifadhia mizigo. |
![]() |
| Hii ndiyo sehemu iliyokuwa na mafundi wa kampuni hiyo walikuwa wakichomelea ndipo cheche za moto zikapenya na kuangukia katika sehemu ya pili ya kuhifadhia mizigo na kuzua motomkubwa. |
![]() |
| Juhudi zikiendelea kwa maafisa wa kikosi hicho kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria. |
![]() |
| Maafisa wa kikosi hicho hapa wamefanikiwa kuzama chini ghalani melini humo kunyunyiza maji zaidi kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria. |
![]() |
| Maafisa wa kikosi hicho hapa wamefanikiwa kuzama chini ghalani melini humo kunyunyiza maji zaidi kuhakikisha moto huo hausambai katika maeneo mengine ya Meli ya Mv Victoria. |








No comments:
Post a Comment