HII NDO SIRI ILYOJIFICHA, KUHUSU AJALI ILIYOTOKEA MBEYA

SIRI ya ajali mbaya ya lori lenye namba za usajili T398 BSE, Scania
Tipa iliyotokea wikiendi iliyopita katika Kijiji cha Mapogolo, Kata ya
Itamboleo, Wilaya ya Mbarali mkoani hapa na kusababisha vifo vya watu
watano na wengine 130 kujeruhiwa vibaya, imefichuka.

Kwa
mujibu wa mashuhuda wa ajali hiyo, lori lililopata ajali lililokuwa
limebeba watu wengi, imevuja kuwa ni mali ya mwekezaji wa shamba la
Kapunga Rice Project na lilikuwa limebeba vibarua wapatao 200, wenyeji
wa Kijiji cha Kapunga waliokuwa wanakwenda kufanya kazi shambani kwake.
Ilidaiwa kuwa dereva wa gari hilo aliyejulikana kwa jina la Baraka
Moleli, alikuwa akiliendesha kwa mwendo wa kasi na alikuwa akijaribu
kuipita pikipiki huku abiria wake wakimshangilia.

Majeruhi
na maiti walipelekwa katika Hospitali ya Mbarali ambapo Mkuu wa Mkoa wa
Mbeya, Abbas Kandoro alifika hospitalini hapo na kusema kuwa katika
ajali hiyo wanaume wanne na mwanamke mmoja walifariki dunia na kati yao
watatu wametambuliwa kuwa ni Samweli Mapugilo Mbena, 30, mkazi wa
Ilembula, Bon Mfupa, 27, mkazi wa Mapogolo na Edger Mwakipesile, 35,
mkazi wa Nonde Mbeya.
No comments:
Post a Comment