Wednesday, February 20, 2013

Jokate Mwegelo azungumzia hisia zake juu ya Penzi la Diamond na VJ Penny

Miss Tanzania namba 02 - 2006, Jokate Mwegelo amezungumzia hisia zake juu ya Penzi la Diamond Platnumz na Mtangazaji wa DTV, VJ Penny. Ambapo pia alikana kwamba alikuwa na urafiki wa karibu na mwanadada huyo kama wengi tunavyoamini.

Jokate ambaye pia ni Mtangazaji wa ‘Channel O’ alikua mpenzi wa Msanii huyo wa Bongofleva (Diamond). Alipotakiwa kuzungumzia hisia zake juu ya Penzi la Diamond na VJ Penny, Jokate alisema:

Anawatakia (Diamond na Penny) kila la kheri na kwamba kawapa baraka zake zote katika uhusiano wao mpya wa kimapenzi kama wamependana na kuridhiana.

“Japokuwa sipendi kumuongelea Diamond lakini ukweli sioni tatizo kwa wao kupendana, mimi naona poa tu.” alimaliza Jokate.

Diamond alikuwa anatoka na Jokate baada ya kuachana na Miss Tanzania namba 01 - 2006, Wema Sepetu. Swala lililoendeleza kutoelewana kwa warembo hao. And now, Diamond gotta a new Chick, VJ Penny!!!

No comments:

Post a Comment