Wednesday, February 20, 2013




Mwanafunzi wa Kidato cha nne amechora ‘Zombie’ kwenye karatasi ya majibu

Katibu Mtendaji wa Baraza la Mitihani Tanzania (Necta), Dk Joyce Ndalichako akionyesha karatasi ya majibu ya mmoja wa watahiniwa wa mtihani wa kidato cha nne wa mwaka 2012, Dar es Salaam jana. 

Mwaka jana pia mwanafunzi mmoja aliandika mashairi ya Bongofleva kwenye karatasi ya majibu, huku akidai kalazimishwa kusoma wakati ana kipaji cha kuimba. Chini ya mchoro huo wa Zombie kumeandikwa;

"Zombie - Amesahau kuvaa viatu."


Katibu mkuu wa baraza la mitihani la taifa, Bi Joyce Ndalichako, amekilaumu kituo cha Radio cha Clouds FM kuwa kilimpa promotion kijana aliendika matusi na "Bongo Flavor" katika mtihani wake wa Kidato cha Nne Mwaka jana kwa kumfanyia interview katika moja ya vipindi vyake.

Katibu mkuu huyo amedai kuwa hatua hiyo ya Clouds FM imechangia uandikaji wa matusi kwa watahaniwa wa mwaka huu.

Hata hivyo, watangazaji wa kituo hicho wamepinga vikali kauli hiyo na badala yake wamemtaka katibu mkuu huyo atoe sababu za kisayansi za kufeli kwa wanafunzi.

No comments:

Post a Comment