Saturday, February 2, 2013

BREAKINGNEWSssssssss JENGO LA PPF TOWER LASHIKA MOTO ASUBUHI HII



Jamani hapa tetemeko limetukumba katika Jengo letu lakini tupo salama ndivyo anavyowasimulia jamaa na ndugu kwa simu huyu dada.(picha  hizi ni  siku  wafanyakazi  wa  jengo hilo  walipotimua mbio kwa  tetemeko)

wafanyakazi wanaotumia jengo hilo wakiwa nje


Habari  kutoka  jijini Dar es Salaam ambazo  zimetua  katika  mtandao huu hivi punde na  kurushwa moja kwa moja na kituo cha radio Nuru Fm 93.5 Mhz  kupitia mwandishi  wetu Dotto Mwaibale  zinadai   kuwa  jengo la PPF TOWER lililopo katikati ya  jiji la Dar es Salaam kwa  sasa  linaendelea kuteketea kwa  moto .

Tukio  hilo  limetokea majira ya saa 1.30 asubuhi  ya leo baada ya  walinzi  wa  jengo hilo  kushuhudia moshi mzito  ukitoka kutoka ndani ya  jengo hilo katika ghorofa  ya mwisho na hivyo kulazimika  kutoa taarifa  vikosi vya zimamoto .

Hata  hivyo  inadaiwa  kuwa  kikosi cha  jeshi la zimamoto na uokoaji  wamefika mapema zaidi  eneo la tukio  na askari  wake  kufanikiwa  kupanda hadi  juu ya ghorofa  hiyo ambako moto huo  ulianzia kuwaka ili kujaribu kuzima japo shida kubwa ni mpira wa maji kufika katika eneo hilo.

Kwani katika  eneo hilo ambako pia kuna mitambo mbali mbali  ya mawasiliano imefungwa  ila mbali ya  kutumia winchi kupandisha mpira  huo wa maji  bado imekuwa ngumu kufika juu ya ghorofa hilo.

Hivyo moja kati ya changamoto ambazo zimetajwa  kwa  wajenzi wa majengo ya ghorofa jijini hapo ni kujenga majengo hayo  huku  wakichukua tahadhari na matukio ya moto  pia .

Mwaibale  amesema  kuwa hadi sasa eneo la  tukio askari  wametanda kila kona ili kupambana  na  vibaka ambao  wamekuwa na kawaida ya   kupora mali katika maeneo ya matukio kama hayo na kuwa hakuna madhara yaliyojitokeza kwa binadamu japo thamani ya mali  zinazoendelea  kuteketea  bado kujulikana na jitihada za kuzima moto  zinaendelea

No comments:

Post a Comment