Saturday, March 30, 2013

KALA JEREMIAH SASA KUJIUNGA BONGO MOVIE, JUA SABABU HAPA

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEgGnIVUe_eBrsEoSqb6s7rEh7PXW0q0-3_K52wM6yqoS-JsJYt-1kpqqm8vKEqNcHI_0KcdqboZMh1DQ7kjhTzgpRLcungFq1hiyhNubLx9nHxHqoyYk6nhtMVLM9vqbFWG37YZ_yKG66o/s1600/Picture+006.jpgMkali wa miondoko ya Hiphop nchini Tanzania ambae anaetamba na kibao cha ‘Dear God’ Kala Jeremiah amefunguka kuhusu mpango wa kufanya movie yake binafsi ambayo huenda ikatoka wakati wowote mapema mwaka huu.

Rapper huyo ambae kwasasa anafanya vizuri na single mpya ya Karibu Dar aliyomshirikisha mkali wa miondoko ya rnb Ben Pol amesema kuwa filamu hiyo ina lengo la kuwapa changamoto vijana wakitanzania kujituma katika shughuli zitakazo waongezea kipato.
Kala Jeremiah ni miongoni mwa rapa wakali waliotokea kwenye shindano la kutafuta vipaji linalosimamiwa na kampuni ya Benchmark Production chini ya mkurugenzi wake Ritha Paulsen

KAULI YA KWANZA BAADA YA LIL WAYNE KUTOKA HOSPITALI NI HII, SOMA HAPA



Rapa Lili Wayne afanya mahojiano na kutoa ufafanuzi wa albamu yake ya 'I'am not a human being'kwa kushindwa kuingia katika orodha ya MTV ya marapa wakali zaidi katika gemu hilo na kuonyesha kuto jali kwa kukosa nafasi hiyo

Lil Wayne alizungumza na kituo cha redio cha power 106 na kufanikiwa kufanya mahojiano yake kwa mara ya kwanza tangu alipolazwa kwa kuzimia mwezi huu

Friday, March 29, 2013

MAJERUHI WA GHOROFA DAR WAFIKIA 18 WANNE WAPOTEZA MAISHA

  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea, huku nondo nyembamba zikionekana na kuacha maswali miongoni mwa mashuhuda wa tukio hilo.
  Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.
 Jitihada za kuwaokoa watu zikiendelea.

Taarifa  zilizotufikia mchana  huu zinadai  kuwa  idadi ya majeruhi  wa ghorofa  lililoporomoka  jijini Dar es Salaam imefikia  18  wakati  watu  wanne  wanadaiwa  kupoteza maisha na jitihada za uokoaji  bado  zinaendelea .

PICHA ZA DIAMOND PLATNUMZ ALIVYOPOKELEWA HUKO KAHAMA::






















ANCELOTTI ATAMANI KUONA BECKHAM AKIBAKI PSG

Carlo Ancellotti Kocha wa PSG amesema anataka kumwona David Beckham akiendelea kuwepo katika klabu hiyo yenye maskani yake Jijini Paris baada ya muda wake kumalizika mwishoni mwa mwezi Juni.


Mchezaji huyo wa zamani wa Manchester United na Kiungo wa Real Madrid alijiunga na timu hiyo mwezi Januari mwaka huu.

Ancelotti amesema Beckham hakukosa katika mazoezi jana dhidi ya Montepellier na kwamba atakuwemo katika kikosi kitakachocheza leo.


PSG ina pointi 58 kileleni mwa Ligi Kuu ya Ufaransa ikifuatiwa na Lyon yenye pointi 53.

MATASHAMASHA YA AIRTEL YATOSHA KUFANYIKA NCHI NZIMA



Kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee moja ya kikundi kitakachotumbuiza katika Matamasha ya Airtel Yatosha akiongea wakati wa uzinduzi wa Matamasha hayo yaliyofanyika katika ofisi za Airtel morocco, Matamasha haya yatawashirikisha wasanii wengine wakiwemo Fid Q, Juma Nature, Ney wa Mitego na Stamina.Kulia Meneja Mauzo Airtel Kanda ya Pwani Raphael Daudi




Meneja Uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando akiongea wakati akitangaza wa Airtel wa kufany Matamasha ya Airtel Yatosha katika mikoa mbalimbali ya Tanzania yenye lengo lan kutoa burudani sambamba na kuelimisha Jamii na wateja wake kuhusu huduma za Airtel ikiwemo kuitambulisha huduma mpya ya Airtel Yatosha. Kulia Meneja Mauzo Airtel Kanda ya Pwani Raphael Daudi

MAirtel Tanzania leo imetangaza mpango wake wa kufanya matamasha ya Airtel Yatosha yenye lengo la kutoa burudani na kuwaelimisha jamii na wateja wake juu ya huduma mbalimbali zinazotolewa na Airtel ikiwemo huduma mpya Airtel Yatosha inayomuwezesha mteja kupiga simu kwenda mtandao wowote kwa gharama nafuu zaidi.


Akiongea wakati wa kutambulisha matamasha hayo, meneja uhusiano wa Airtel Bwana Jackson Mmbando alisema “Airtel tumeamua kutoa burudani wakati wa msimu huu wa sikukuu ikiwa ni pamoja na kuitambulisha huduma yetu ya Airtel yatosha kwa watanzania, tunaamini kwa kupitia matamasha yatakayofanyika katika mikoa mbalimbali ya Tanzania wateja wetu na watanzania kwa ujumla watapata burudani na kupata nafasi ya kupata elimu juu ya huduma zetu Nyingi



“Safari yetu ya burudani za Airtel yatosha itaanza katika Mkoa wa Morogoro katika siku ya Jumapili na Jumatatu ya Tarehe 31/3 na 01/04/2013, Kuanzia Saa Tatu kamili Asubuhi mpaka saa Kumi na Mbili Jioni, pale katika viwanja vya Sabasaba.


Tutakuwa na wasanii mbalimbali wakiwemo Fid Q, Juma Nature, Ney wa Mitego na Tip Top Connection. Kiingilio ni BURE , tunapenda kukukualika wewe na washikaji zako wote kuhudhuria katika tamasha hili la kwanza kabisa pale morogoro na utape burudani kabambe. Njoo na Kitambulisho chako ili uunganishwe na ufurahie ofa nyingi toka Airtel” aliongeza Mmbando .


Naye kiongozi wa Tip Top connection Bwana Madee alisema” kama kawaida tumejipanga kuwapa wateja wa Airtel na watanzania burudani ya Ukweli katika mikoa mbalimbali ya Tanzania, tunaomba watanzania wajitokeze kwa wingi katika matamasha haya ya Airtel Yatosha. Mbali na sisi kutoa burudani itakuwa nafasi pia kwetu kuona vipaji mbalimbali vya mashabiki wetu ambao ndio wasanii nyota wa kesho hivyo tuwapa hamasa ya kujitokeza kwa wingi ili tuweze kuburudika pamoja.


Wasanii watakaoshiriki katika Matamasha maalumu ya Airtel yatosha watatumbuiza kwa vibao vyao mahiri kama vile Fid Q na kibao chake cha Sihitaji Marafiki na Ney wa Mitego na kibao chake cha Nasema Nao huku Tip Top Connection wakiwakilisha na kibao chao cha Nani kamwaga pombe yangu.


Airtel hivi karibuni imezindua huduma ya Airtel Yatosha inayomuwezesha mtumiaji wa mtandao wa Airtel kupiga simu kwenda mitandao yote kwa gharama ya chini kabisa na hivyo kutokuwa na haja tena ya kubadilisha kadi ya simu pindi anapohitaji kuongea na mtu wa mtandao mwingine. Mteja anajiunga kwenye huduma hii kwa kupiga *149*99#

PICHA ZAIDI ZA JENGO LILILOPOROMOKA LEO HII

.
Mabaki ya jengo hilo lililoporomoka jijini da es salaam amablo lipo barabara ya morogoro mtaa wa indiana.Endelea kupitia audifacejackson blogspot kwa taarifa ziadi .

Wananchi waliokuwa eneo la tukio kwa ajili ya kusaidia kukoa wakijitahidi bila mafanikio kwa kuwa hapa ni lazima kuwepo na vifaa vya kunyanyua vitu vizito ili kurahisisha zowzi la kuokoa.


Monday, March 11, 2013

BAADA YA MISUKUSUKO MINGI WASTARA SASA KWENDA KUPUMZIKA UARABUNI


http://www.bongocinema.com/images/casts/wastara_juma.jpg 
MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood Wastara Juma ‘Stara’ amesema kuwa baada ya muda mwingi wa mihangaiko ya kuuguza na hata kumpoteza mumewe anahitaji kupumzika na kujenga akili upya.

Katika kulifanya hilo ameamua kwenda kupumzika Uarabuni kwa ajili ya kutuliza akili na kujipanga upya, akiongea na BK COP amesema kwa sasa anahitaji kupumzika kwa muda…!!!!!

TFF YASEMA BADO TANZANIA HAIJAFUNGIWA ILA SERIKALI IKIENDELEA KUINGILIA SHUGHULI ZAO FIFA KUIFUNGIA TANZANIA

Shirikisho la Kimataifa la Vyama vya Mpira wa Miguu (FIFA) limesema litaifungia Tanzania iwapo itabainika kuwa Serikali imekuwa ikiingilia shughuli za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
FIFA imesema kumekuwa na shutuma kupitia taarifa mbalimbali za vyombo vya habari nchini kuwa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo imeonesha nia ya kuingilia uendeshaji wa TFF.
Kwa mujibu wa barua ya jana (Machi 10 mwaka huu) ya FIFA kwenda kwa Rais wa TFF, Leodegar Tenga, vyombo vya habari vimemkariri Waziri (Dk. Fenella Mukangara) kuwa Serikali imeiagiza TFF kutumia Katiba ya mwaka 2006 katika uchaguzi wakati tayari imeshafanyiwa marekebisho.
“Pia imeelezwa kuwa TFF imetakiwa kufanya Mkutano Mkuu pamoja na ule wa uchaguzi kwa tarehe ambazo zimepangwa na Serikali. Vilevile imeelezwa kuwa Serikali inakusudia kuunda Kamati ya Muda iwapo TFF haitatekeleza maagizo yake,” imesema sehemu ya barua hiyo iliyosainiwa na Katibu Mkuu wa FIFA, Jerome Valke.
FIFA imesema iwapo yaliyoripotiwa na vyombo vya habari yatathibitika kuwa kweli, maana yake huo ni uingiliaji wa wazi wa Serikali kwa shughuli za TFF.
“Tunapenda kuwakumbusha kuwa wanachama wote wa FIFA wanatakiwa kuendesha shughuli zao kwa uhuru bila kuingiliwa na mtu mwingine kama ilivyoelezwa katika ibara za 13 na 17 za Katiba ya FIFA.
“Hivyo kama maagizo hayo yanayodaiwa kutolewa na Serikali yatatekelezwa, suala hili litapelekwa katika mamlaka za juu za FIFA kwa hatua zaidi ikiwemo kuisimamisha Tanzania kama ambavyo inakuwa pale panapokuwa na uingiliaji wa Serikali,” imesema barua hiyo.
Barua hiyo ambayo nakala yake pia imetumwa Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) imeelezea baadhi ya athari ambazo Tanzania itakumbana nazo endapo itasimamishwa ni timu za taifa pamoja na klabu kutoshiriki mechi za kimataifa kwa mujibu wa Ibara ya 14 ya Katiba ya FIFA.
Vilevile si TFF au wanachama wake na maofisa wengine watakaoweza kunufaika na programu za maendeleo, kozi au mafunzo yanayotolewa na FIFA na CAF.
“Madai ya uamuzi uliofanywa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo ni ya kusikitisha kutokana na ukweli kuwa FIFA ilishatangaza itatuma ujumbe wake kuchunguza jinsi hali ilivyo kwa sasa na kutoa mapendekezo yake. Kutokana na hali hii, ujumbe wa FIFA uliokuwa uje kuchunguza (suala la uchaguzi) itabidi usubiri kwa vile ni muhimu kushughulikia tatizo hili kwanza.
“Katika mazingira haya tunaomba ueleze msimamo huu wa FIFA kwa mamlaka zinazohusika (Serikali) na athari ambazo mpira wa miguu wa Tanzania utakumbana nazo. Tunakushuru na tunatarajia utatufahamisha kila hatua inayoendelea katika suala hili,” imesema barua hiyo.
MEHRA OMARY.................................

DIAMOND: MSIMAMO WANGU WA KUJENGA MSIKITI BADO UKO PALE PALE

Ikiwa imepita mda sasa tangu alipogusia swala la kujenga msikiti, ambao utakuwa kumbukumbu yake kwa watakaoutumia, na ikiwa ni njia moja wapo ya kurudisha katika jamii, Diamond amesema msimamo wake bado uko palepale 
"sasa hivi mimi nina maeneo yangu, kwasababu ninapikuwa na hela mi nakuwa muoga sana kuwekeza najitahidi sana kununua nunua viwanja au kama hivi vijumba vidogo vidogo vya kuvunja maeneo tofauti tofauti, sasa hivi niko plani kwamba niujengee sehem gani, nitengeneze msikiti sehem ambayo itakua ni nzuri, msikiti ambao hata kesho na kesho kutwa mi nikifa, mababu vizazi na vizazi viwe wanaswali pale kama msikiti ambao aliutengeneza kijana wetu Diamond, na watu wanaswalia, mi naamini  itanipa baraka kubwa sana, na soon too naimani mwenyezi mungu naimani atanisaidia, nitangeneza huo msikiti" amesema Diamond
licha ya kuwa na plani ya kujenga mskiti huo, iliripotiwa kuwa kwa sasa ameshakamilisha ujenzi wa nyumba ya mama yake mzazi iliyogharimu zaidi ya shilingi ta kitanzania milioni 260..

POMBE YA ULANZI YATOA AJIRA KWA VIJANA IRINGA

 Vijana  wachuuzi  wa  pombe ya kienyeji aina ya Ulanzi inayotokana na mimea aina ya mianzi wakisafirisha  pombe  hiyo kutoka vijijini kuelekea  mjini Iringa ,debe moja huuzwa kwa TSh 2500
 Vijana  wachuuzi wa pombe aina ya ulanzi  wakiwa katika baiskeli  zao  huku kushoto ni kijana kibarua akifukuza  ili kupata ajira ya  kusukuma baiskeli mlimani kwa  ujira wa Tsh 200 kwa kila Baiskeli 
 Ulanzi umeweza kutoa ajira kwa vijana mkoani Iringa kama wanavyoonekana hawa  pichani  wakiwa katika ajira yao na kuajiri wengine pia

DAR ES SALAAM MCHANA WA LEO

 Ajali  hii imetokea  jirani kabisa la makao makuu ya kampuni ya Airtel Tanzania  eneo la Moroco jijini Dar es Salaam mchana wa leo kabla ya  mvua  kuanza  kunyesha ,baada ya  dereva  wa lori  hili kushindwa kulimudu vema gari lake na kujikuta anatumbukia katika mtaro

 Mashuhuda  wakishuhudia ajali  hiyo ambayo hata  hivyo haijkasababisha madhara kwa binadamu

GARI YA KIKOSI CHA KUZIMA MOTO MBOZI LAGEUZWA GARI YA MATANGAZO KWENYE MIKUTANO WILAYANI HUMO

HAPA MAFUNDI WAKIWA NDANI WAKIANDAA VIPAZA SAUTI
FUNDI MITAMBO AKIENDELEA KUNYOOSHA WAYA
SASA KAZI IMEANZA  TUOMBE MOTO USITOKEE MAANA SIJUI ITAKUWAJE JIBU MNALO WENYEWE 

KWA WAPENZI WA GENEVIEVE NA OMOTOLA, HIVI NDO VIWALO WALIVYOTOKELEZEA NAVYO AMVC



Sunday, March 10, 2013

PICHA ZA UCHI ZA MSANII SAPNA ALIYETOKELEZEA KATIKA VIDEO YA JAMBO JAMBO YA STEVE RnB

WAKATI mabinti wengi hasa mastaa wa Bongo wakijuta baada ya picha zao za utupu walizopigwa na wapenzi wao kuvuja, kwa msanii mrembo aliyepamba video ya wimbo wa Bongo Fleva uitwao Jambojambo wa msanii Steve R&B,
Aisha Firozi ‘Sapna’ ni kawaida kwani hujifotoa mwenyewe.
Chanzo makini cha Risasi  kimewasilisha folda lenye picha za kutosha za mrembo huyo akiwa mtupu huku kikieleza kwamba ni mchezo wake kujipiga mwenyewe picha hizo.  
Kwa sharti la kutochorwa jina lake , chanzo hicho ambacho kipo  aribu na Sapna kilisema: “Yule ni mtu wangu wa karibu sana, lakini tabia yake kwa kweli huwa siipendi kabisa. Anajipiga picha chafu mwenyewe, kwake ni starehe kubwa, huwezi kuamini.”
  Kikiendelea  ufunguka zaidi, chanzo hicho kilipasha kuwa, picha hizo amejipiga hivi karibuni nyumbani kwa rafiki yake aitwaye Doreen, Tabata - Magengeni jijini Dar es Salaam, ambapo alikuwa akiishi naye.
KAULI YA  SAPNA.....
Ukistaajabu ya Musa utayaona ya Firauni; Sapna alipopigiwa simu  na kuelezwa kuhusu kunaswa kwa picha hizo, kwanza alishangaa lakini akakiri kuzitambua.

“Hizo kweli ni picha zangu na nilijipiga mwenyewe sasa sijui wewe umezipataje na zimefi kaje huko kwenu? Mimi nilipiga kwa masilahi yangu mwenyewe, huwa natamani sana kujiangalia jinsi umbo langu lilivyo, ndiyo maana niliamua kujipiga na si vinginevyo.

“Kila mtu na maisha yake na mimi sikuwa na dhamira mbaya kujipiga picha hizo zaidi ya kujiangalia tu nilivyo,” alisema Sapna.