KALA JEREMIAH SASA KUJIUNGA BONGO MOVIE, JUA SABABU HAPA
Mkali wa miondoko ya Hiphop nchini Tanzania ambae anaetamba na kibao cha
‘Dear God’ Kala Jeremiah amefunguka kuhusu mpango wa kufanya movie yake
binafsi ambayo huenda ikatoka wakati wowote mapema mwaka huu.Rapper huyo ambae kwasasa anafanya vizuri na single mpya ya Karibu Dar aliyomshirikisha mkali wa miondoko ya rnb Ben Pol amesema kuwa filamu hiyo ina lengo la kuwapa changamoto vijana wakitanzania kujituma katika shughuli zitakazo waongezea kipato.
Kala Jeremiah ni miongoni mwa rapa wakali waliotokea kwenye shindano la kutafuta vipaji linalosimamiwa na kampuni ya Benchmark Production chini ya mkurugenzi wake Ritha Paulsen
No comments:
Post a Comment