Thursday, March 7, 2013

HILI NDILO DAU LA WAYNE ROONEY ANALOTARAJIWA KUUZWA


Manchester United wanafikiria kumuuza Wayne Rooney kwa kiasi cha pound milioni 35. Kuna maongezi kati ya Man u na Real Madrid kuhusu Wayne Rooney kwenda kuichezea Real Madrid msimu ujao.
Inaovyoneka Mabingwa hao wa uingereza wanafikiria jinsi ya kumrudisha Christiano Ronaldo Manchester United. Wiki iliyopita gazeti la Times lilisema kwamba Paris Saint-Germain ndio timu ambayo imeonyesha nia ya kumtaka mshambuliaji huyo wa Manchester United

Pia Manchester United bado wataendeleza nia yao ya kumsajili mshambuliaji kutoka Borussia Dortmund Robert Lewandowski ambaye pia inasemekana ndiye atakaye ziba pengo la Wayne Rooney endapo watashindwa kumrudisha Christiano Ronaldo.
Mtandao wa ESPN pande za uiengereza umesema kwamba Manchester United watapoteza kiasi cha pound millioni 22 kutokana na kutolewa katika hatua za mtoano na Real Madrid.

No comments:

Post a Comment