KIJANA ACHOMWA KISU AKITOKA KUPATA STAREHE ZA MWISHO WA WIKI
kijana Godfrey Masharo mkazi wa
mjini Iringa akivuja damu baada ya kuchomwa kisu kifuani na watu
wasiofahamika usiku wa leo wakati akitoka kujirusha disco
Hapa akivuja damu akiwa nje ya kituo cha polisi kabla ya kupelekwa hospitali ya mkoa wa matibabu zaidi
Hivi ndivyo alivyochomwa kisu kijana huyo.
...........................................................................................................................................................
WATU wasiofahamika wamemvamia na
kumchoma na kitu chenye ncha kali kifuani mkazi wa mjini Iringa
Godfrey Masharo (pichani) .
Tukio hilo limetokea jana usiku
majira ya saa 11 alfajiri wakati kijana huyo akitoka kujirusha
katika kumbi za starehe mjini hapa.
Akizungumza kwa tabu na mtandao huu
wa www.francisgodwin.blogspot.com kijana huyo anadai kuwa watu hao
watatu ambao hawafahamiki kwa majina walimvamia na kumchoma na kitu
hicho chenye ncha kali kifuani na kukimbia .
Alisema kuwa tukio hilo limetokea
eneo la Miyomboni barabara kuu ya Iringa -Dodoma jirani na jengo la
Hazina Ndogo ya mkoa wa Iringa .
Hata hivyo alisema kuwa msaada
wake ulitoka kwa wasamaria wema ambao walimkuta eneo hilo akiwa
ameanguka kwa kupoteza fahamu na kukimbizwa katika kituo cha polisi
kabla ya kupelekwa Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu
zaidi .
No comments:
Post a Comment