MATOKEO YA UCHAGUZI KENYA .UHURU MWENDO MDUNDO

Tume ye uchaguzi inaendelea kutoa matokeo ya uchaguzi wa kihistoria Kenya
Baada ya siku ndefu ya watu
kupiga kura nchini Kenya, wengi wana hamu kujua rasmi mshindi wa
uchaguzi wa urais. Hata hivyo matokeo ya mwanzo yameanza kutolewa na
tume ya uchaguzi na mipaka Kenya, IEBC.
Matokeo hadi kufikia saa kumi na mbili jioni yalikuwa yanaonyesha Uhuru Kenyatta
akiongoza dhidi ya mpinzani wake Raila Odinga. Matokeo kutoka sehemu
mbali mbali yalichelewa hasa kwa sababu ya hitilafu za kimitambo.
17:31Ng'endo Angela aliye katika eneo bunge la Othaya anasema kuwa Mary Wambui amemrithi rais mstaafu Mwai Kibaki kama mbunge wa eneo bunge la Othaya baada ya miaka 39 ya Kibaki kuwa mbunge wa eneo hilo. Kibaki alikuwa amempendeka Mugambi Manyara kuwa mrithi wake, lakini ameshikilia nafasi ya tatu
17:29 Matokeo ya mwanzo mwanzo ya kura za urais yaliyotolewa sasa hivi kutoka kwa tume ya uchaguzi yanaonyesha kuwa Raila Odinga ana kura 2,133,202 wakati Uhuru Kenyatta ana kura 2, 718,021
17:05 Kwa sasa Raila Odinga ana kura 2, 107, 670 wakati Uhuru Kenyatta akiwa na kura 2,697,056
17:02 Vigogo wa Muungano wa
CORD wake Raila Odinga wamesema kuwa licha ya matokeo kuonyesha bado
wako nyuma, wafuasi wao wasiwe na wasiwasi kwani kura nyingi zingali
kuhesabiwa. Mgombea mwenza wake Kalonzo Musyoka amewaambia
wapiga kura kupitia televisheni kuwa wawe watulivu wasubiri matokeo kutoka kwa tume ya uchaguzi
15:00 Matokeo kufikia sasa ni kwamba Uhuru Kenyatta amepata kura 2,606,617 wakati Raila odinga ana kura 2,011,869
14:31 Hadi kufikia sasa kulingana na matokeo yanayotolewa na Tume huru ya uchaguzi Kenya ni kuwa Uhuru Kenyatta amepata kura 2,534 019 wakati Raila Odinga akiwa na kura 1,939,549. Haya ni matokeo ya mapema tu
No comments:
Post a Comment