WAFANYABIASHARA WA KITIMOTO IRINGA WAPINGA KUFUNGIWA BIASHARA
Hapa wakiamua kuchimba barabara kuzuia magari kupita eneo hilo
Maandamano ya kupinga marufuku ya uuzaji wa kitimoto leo
Wafanyabiashara wa kitimoto katika
eneo la vibanda vya UVCCM mjini Iringa leo wamewatimua mgambo wa
Manispaa ya Iringa ambao wamefika eneo hilo kufunga biashara zao kama
njia ya kunusuru wananchi na ugonjwa wa homa ya nguruwe.
Tukio hilo limetokea leo majira ya
saa 12 jioni baada ya ofisa mifungo Manispaa ya Iringa akiwa na
mgambo kufika eneo hilo kufunga biashara zote za kitimoto eneo
hilo.
wakizungumzia hatua hiyo
wafanyabiashara hao wamesema kuwa wanashangazwa na uamuzi huo wa
uongozi wa afya Manispaa ya iringa kuwazuia wao kufanyabiashara
hiyo wakati maeneo mbali mbali maarufu nyama hiyo ikiendelea kuuzwa
kama kawaida .
Hivyo wameutaka uongozi wa Manispaa
ya Iringa kusitisha mpango huo kwani unawatesa wananchi hao
wajasiriamali wenye kipato cha chini ambao wanategemea biashara hiyo.
No comments:
Post a Comment